Habari Za Un

Informações:

Synopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodes

  • Jifunze Kiswahili: Tofauti ya maneno “Adhiri na hadhiri.”

    18/04/2024 Duration: 01min

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adhiri; na  hadhiri.”

  • 18 APRILI 2024

    18/04/2024 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina amabyo hivi karibuni tulizungumza na Peter Mmbando kutoka Tanzania akifafanua nini wanafanya ili kuimarisha matumizi endelevu ya teknolojia ya kidijitali. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi na tofauti ya maneno “Adhiri; na  hadhiri."Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameelezea hofu yao juu mwenendo wa mashambulizi dhidi ya shule, vyuo vikuu, waalimu na wanafunzi kwenye Ukanda wa Gaza hali ambayo wamesema ni ishara ya mpango wa uharibifu mkubwa wa mfumo wa elimu wa Palestina.Muungano wa chanjo duniani GAVI na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wamekaribisha taarifa kwamba chanjo mpya ya matone ya kipindupindu Euvichol-S, sasa imepokelewa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na inaweza kupatikana katika nchi mbalimbali duniani. Kupitishwa kwa chanjo hiyo mpya kutasaidia kuongeza usambazaji wake kwa takriban dozi milioni 50 mwaka huu ikilinganishwa na dozi milioni 38 zilizosambazwa mwaka 2023.  Mkutano wa Wiki ya Ue

  • Vijana wakiwezeshwa wanaweza kuvumbua teknolojia ya kusongesha malengo ya maendeleo endelevu

    17/04/2024 Duration: 08min

    Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika jukwaa la vijana la Baraza la kiuchumi na kijamii ECCOSOC ambalo linatoa ukumbi wa kimataifa wa mazungumzo kati ya nchi wanachama na viongozi vijana kutoka kote ulimwenguni kujadili suluhu za changamoto zinazoathiri ustawi wa vijana. Hafla hii pia hutumika kama nafasi ya kipekee kwa vijana kushiriki maono na hatua zao ili kuharakisha utekelezaji wa Ajenda ya 2030 na SDGs ikiwemo masuala ya uvumbuzi na teknolojia. Miongoni mwa wanaohuduria jukwaa hilo kutoka Tanzania ni Vivian Joseph Afisa tabibu na mkuu wa wa kitengo cha afya akiwasilisha vijana katika jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC na Joramu Nkumbi mkurugenzi mtendaji wa jukwaa la Afrika la viongozi vijana kwa upande wa Tanzania. Wameketi na Flora Nducha na kumweleza walichoambulia hadi sasa katika jukwaa hilo litakalokunja jamvi kesho..

  • Mapigano na mizozo DR Congo yanyima wananchi manufaa ya utajiri wa nchi yao - Türk

    17/04/2024 Duration: 02min

    Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk ambaye yuko katika ziara rasmi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amestaajabu ni kwa vipi utajiri wa maliasili uliosheheni kwenye taifa hilo umeleta manufaa kidogo kwa wananchi wako kutokana na ghasia na mapgano. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Video ya Umoja wa Mataifa inaanzia Kinshasa mji mkuu wa DRC ambako Bwana Türk na aafisa mmoja wa Umoja wa Mataifa wanatazama ramani ya taifa hilo lililoko Maziwa Makuu na kisha anasema ni moja ya nchi tajiri zaidi duniani, lakini tunaona ni kwa vipi utajiri huu kwa bahati mbayá hauko kunufaisha wananchi kwa sababu ya mapigano.Na kisha anaelezea mipango ya ziara yake ya kutathmini hali ya haki za binadamu akisemakwanza ni kukutana na watu waliofurushwa makwao kutokana na ghasia na vile vile kuonana na mamlaka husika na mashirika ya kiraia.Baada ya hapo safari inaanza akiambatana na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Bintou Keita, mwelekeo ni Mashariki mwa nchi

  • 17 APRILI 2024

    17/04/2024 Duration: 13min

    Hii leo jaridani tunaangazia ghasia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na jitihada za Umoja wa Mataifa za kukwamua hali ya Kibinadamu nchini Ethiopia. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunaelekea nchini Madagascar, kulikoni?Kaminshna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk ambaye yuko katika ziara rasmi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amestaajabu ni kwa vipi utajiri wa maliasili uliosheheni kwenye taifa hilo umeleta manufaa kidogo kwa wananchi wako kutokana na ghasia na mapgano.Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Kutoa ahadi kwa ajili ya ufadhili wa kukwamua hali ya Kibinadamu nchini Ethiopia uliokamilika jana mjini Geneva, Uswisi umetangaza kwamba wafadhili 20 wametangaza msaada wa kifedha wa Dola za Marekani milioni 610 angalau kuhakikisha misaada kwa miezi michache ijayo.  Makala inaturejesha hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kunakofanyika jukwaa la vijana la Baraza la kiuchumi na kijamii ECCOSOC ambalo linatoa ukumbi wa kimataifa wa mazungumzo kati ya nch

  • Mkutano wa ufadhili wapata msaada wa fedha wa dola milioni 610 kwa ajili ya Ethiopia

    17/04/2024 Duration: 01min

    Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Kutoa ahadi kwa ajili ya ufadhili wa kukwamua hali ya Kibinadamu nchini Ethiopia uliokamilika jana  mjini Geneva, Uswisi umetangaza kwamba wafadhili 20 wametangaza msaada wa kifedha wa Dola za Marekani milioni 610 angalau kuhakikisha misaada kwa miezi michache ijayo.Mkutano huo uliolenga kukusanya dola bilioni 1 za kimarekani kwa ajili ya miezi mitano ijayo, ulikuwa umeandaliwa kwa pamoja kati ya Umoja wa Mataifa, Serikali ya Ethiopia na Uingereza, na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa masuala ya kibinadamu.  Mara tu baada ya mkutano huo Naibu Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura OCHA, Joyce Msuya, aliwashukuru wafadhili hao na kusema kuwa huo ni mwanzo tu na matumaini ni kuendelea na kuongeza msaada kwa mwaka mzima.Dharura ya kibinadamu nchini Ethiopia imekuwa ikiongezeka kupitia mizunguko ya ukame na mafuriko, na migogoro. Ukosefu wa uhakika wa chakula na utapiamlo unatarajiwa kufikia kiwango cha juu kwa watu milioni 10.8 wakati

  • 16 APRILI 2024

    16/04/2024 Duration: 12min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Tanzania, Abeida Rashid Abdallah anafafanua kwa nini Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Zanzibar ni chanda na pete.  Pia tunakuletea muhtasari ya habari na mashinani kama zifuatazo.Leo mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kuonya juu ya vita inayoendelea kukatili maisha ya watu Gaza, na kusambaratisha miundombinu yakitaja kuwa wanawake karibu 10,000 wamepoteza Maisha tangu vita kuanza miezi sita iliyopita huku mtoto mmoja anajeruhiwa au kuuawa kila dakika 10.Jukwaa la vijana la Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC leo limeng’oa nanga hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Matrekani likiwaleta maelfu ya vijana kutoka kila kona ya Dunia. Joramu Nkumbi ni miongoni mwa washiriki wa jukwaa hilo kutoka Tanzania na anafafanua wanachokijadili mwaka huu.  Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM kwa shirikiana na mashirika mengine 48 y

  • Ni dhana potofu kudai Wamaasai wanaua Simba ili kupata mke - Alois Porokwa

    15/04/2024 Duration: 03min

    Katika harakati za kupambana na mabadiliko ya tabianchi, kuna wakati jamii ambazo bado zinaishi kiasili zimekuwa zikilaumiwa kwamba zinachangia kuharibu mazingira kutokana na wao kuishi katika mazingira fulani; mathalani misitu na mbuga jambo ambalo linakanushwa na jamii hizo wakidai kwamba kimsingi wao ndio watunzaji wazuri wa mazingira kwani wanayategemea moja kwa moja kwa mustakabali wa maisha yao ya kila siku na siku zijazo. Hivi karibuni wakati wa Mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6 uliofanyika jijini Nairobi, Kenya, Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Kenya, Stella Vuzo alimhoji Alois Porokwa, Mkurugenzi wa shirika la NALEPPO kutoka jamii ya Wamaasai aliyesafiri kutoka Kijiji cha Emboreet, Wilaya ya Simajiro, Mkoa wa Manyara, Tanzania. Ni katika mazungumzo hayo ndipo Stella Vuzo akakumbuka kumuuliza Alois Porokwa swali hili ambalo ni dhana inayohusisha jamii ya Wamaasai kuua wanyama.

  • Jukwaa la Jamii za watu wa asili lafungua pazia katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa

    15/04/2024 Duration: 01min

    Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa jijini New York Marekani, Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili limeanza rasmi na litadumu kwa muda wa wiki mbili likiwaleta pamoja zaidi ya washiriki 2000 wa jamii za asili kutoka kila pembe ya dunia kujadili masuala mbalimbali. Hiki ni kikao cha 23 cha jukwaa hili la kudumu la watu wa jamii za asili ambao leo mkutano wa kwanza umefunguliwa rasmi ukihudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa akiwemo Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Balozi Dennis Francis. Majadiliano ya wiki mbili za mkutano huu yataongozwa na dhima ya kuangazia haki za watu wa asili kujitawala pamoja na sauti za vijana wa jamii ya asili. Sehemu muhimu ya majadiliano haya inalenga kuhakikisha watu wa jamii za asili wanapata haki ya kujiamulia na kupata ufadhili utakao wawezesha kudai haki zao vyema, kuendeleza maendeleo yao ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni na kufadhili miundo ya utawala wao, kama ilivyoainishwa katika Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu

  • 15 APRILI 2024

    15/04/2024 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia utekwaji nyara wa watoto wa kike 275 huko Chibok nchini Nigeria, na uwezeshaji kiuchumi wa watu wa asili. Makala inamulika masuala ya mazingira ikiangazia watut wa asili na mchango wao, na mashinani tunakupeleka nchini Chad kusikia simuliza ya mkimbizi kutoka Sudan.  Nigeria inapotimiza miaka 10 tangu tukio la utekwaji nyara la watoto wa kike 275 huko Chibok, kaskazini magharibi mwa taifa hilo, hadi sasa bado watoto 90 wamesalia mateka na nchi hiyo inasalia na kumbukumbu ya tukio linguine la wanafunzi wa shule kutekwa nyara jimboni Kaduna mwezi Machi mwaka huu, hali inayosababisha Umoja wa Mataifa kutoa wito mahsusi.Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa jijini New York Marekani, Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili limeanza rasmi na litadumu kwa muda wa wiki mbili likiwaleta pamoja zaidi ya washiriki 2000 wa jamii za asili kutoka kila pembe ya dunia kujadili masuala mbalimbali. Makala Stella Vuzo, Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Matai

  • UNICEF: Miaka 10 ya watoto kutekwa Chibok, bado hakuna mifumo ya ulinzi

    15/04/2024 Duration: 02min

    Nigeria inapotimiza miaka 10 tangu tukio la utekwaji nyara la watoto wa kike 275 huko Chibok, kaskazini magharibi mwa taifa hilo, hadi sasa bado watoto 90 wamesalia mateka na nchi hiyo inasalia na kumbukumbu ya tukio linguine la wanafunzi wa shule kutekwa nyara jimboni Kaduna mwezi Machi mwaka huu, hali inayosababisha Umoja wa Mataifa kutoa wito mahsusi.  Ilikuwa usiku wa tarehe 15, Jumatatu ndipo watoto hao wa kike wenye umri wa kati ya miaka 12 hadi 17 walitekwa na kundi la Boko Haram huko jimboni Borno, na ndio maana kwa mazingira yalivyo sasa, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema safari bado ni ndefu kwa watoto nchini Nigeria kutimiza ndoto yao ya kusoma kwenye mazingira yaliyo salama, kwani ni asilimia 37 tu ya shule kwenye majimbo 10 yaliyo kwenye mazingira hatarishi ndio zina mifumo ya kubaini mapema vitisho kama vile shule kushambuliwa. Ripoti ya UNICEF iliyotolewa leo Abuja, miji Mkuu wa Nigeira ikipatiwa jina Viwango vya Chini Vya Usalama Shuleni au MSSS kwa lugha ya kiing

  • Guterres/Kwibuka 30: Vijana kemeeni kauli za chuki kokote muisikiapo na muionapo

    12/04/2024 Duration: 03min

    Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Baraza Kuu limekuwa na tukio maalum la kumbukizi ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda au KWIBUKA30, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo, Antonio Guterres ametumia hotuba yake pamoja na mambo mengine kuwasihi vijana kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki kukemea chuki kokote wanapoisikia au kuiona. Tukio lilianza kwa ukumbi kuwa giza na video ya dakika tano ikachezwa kueleza kuwa watu wengi wanaijua Rwanda kuanzia 1994, lakini ilikuweko hata kabla ya ukoloni, na kwamba wakoloni ndio waligawa watu kwa misingi ya makundi licha ya kwamba lugha yao ilikuwa moja. Manusura na watekelezaji wa mauaji walizungumza pia kwenye video hiyo!Video ikafuatiwa na kuwasha mishumaa kukumbuka waliouawa na kisha hotuba ambapo Katibu Mkuu Guterres akawa ana ujumbe mahsusi kwa vijana wa Rwanda walioshiriki kimtandao na pia ukumbini.Anasema rafiki zangu, katu hatutasahau vitisho vya siku 100. Lakini tunahitaji msaada wenu. Tunahitaij sauti na uchechemuzi wenu kusongesha kumbukizi z

  • Kikosi cha 11 cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT-11 watoa matibabu kwa raia nchini DRC

    12/04/2024 Duration: 03min

    Kikosi cha 11 cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT-11 kinachohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO wametekeleza wajibu wao wa kulinda raia kwa kuwapatia huduma ya matibabu kwenye Kijiji cha Matembo kilichoko mjini Beni jimboni Kivu Kaskazini. Shuhuda wetu ni Kapteni Fadhila Nayopa, Afisa habari wa kikosi hicho. 

  • 12 APRILI 2024

    12/04/2024 Duration: 13min

    Hii leo jaridani tunaangazia kumbukizi wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, na wakimbizi wa Sudan wanaovuka mpaka kuelekea nchini Sudan Kusini. Makala na mashinani tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Baraza Kuu limekuwa na tukio maalum la kumbukizi ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda au KWIBUKA30, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo, Antonio Guterres ametumia hotuba yake pamoja na mambo mengine kuwasihi vijana kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki kukemea chuki kokote wanapoisikia au kuiona.Tarehe 15 April wiki ijayo siku ya jumatatu nchi ya Sudan itatimiza mwaka mmoja rasmi tangu kuanza kwa mzozo kati ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na Vikosi vya jeshi la Sudan (SAF). Vita hiyo imesababisha maelfu ya watu kuwa wakimbizi wa ndani na wengine kusaka hifadhi nchi Jirani. Mashirika ya misaada ya kibinadamu nayo yamekuwa mstari wa mbele kusaidia wananchi wenye uhitaji japo yanakabiliwa na ufinyu wa bajeti. Makala tunakupelek

  • Wakimbizi kutoka Sudan wanoingia Sudan Kusini wanaendelea kuongezeka

    12/04/2024 Duration: 02min

    Tarehe 15 April wiki ijayo siku ya jumatatu nchi ya Sudan itatimiza mwaka mmoja rasmi tangu kuanza kwa mzozo kati ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na Vikosi vya jeshi la Sudan (SAF). Vita hiyo imesababisha maelfu ya watu kuwa wakimbizi wa ndani na wengine kusaka hifadhi nchi Jirani. Mashirika ya misaada ya kibinadamu nayo yamekuwa mstari wa mbele kusaidia wananchi wenye uhitaji japo yanakabiliwa na ufinyu wa bajeti.Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP inaanza kwa kuonesha wananchi wakiwa na vifurushi mikononi, wengine wakiwa wamepanda usafiri unaosukumwa na ngombe na wengine mabasi wakiingia katika mpaka wa Joda nchini Sudan kusini wakitokea nchini Sudan.“Tumesafiri kwakutumia basi na imetuchukua siku mbili kufika hapa”, ndivyo anavyosema Hamida Ibrahim mkimbizi kutoka Sudan. Anaendelea kwa kueleza kile wanachohitaji kwa sasa. “Tunahitaji chakula. Huo ndio msaada wa haraka tunaohitaji ili tuweze kuishi. Kwa sababu tupo na watoto na hawana uwoga wanachojua wanakuja hapa kuf

  • 11 APRILI 2024

    11/04/2024 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Alice Nderitu, Mshauri Maalum wa Umoja wa Mataifa katika kuzuia mauaji ya kimbari akiwa Kigali hivi majuzi kwenye kumbukizi anamulika nini kifanyike kuhakikisha kitendo kama hicho kinasalia historia. Pia tunakuletea muhtasari wa habari za Gaza, Sudan, Uganda na uchambuzi wa neno “PAMBAJIO”.Wakati mgogoro nchini Sudan ukiingia katika mwaka wake wa pili, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kutafuta Ukweli nchini Sudan umezitaka pande zinazokinzana zisitishe mapigano, zilinde raia na kuruhusu mtiririko wa misaada. Taarifa iliyochapishwa leo na OHCHR imemnukuu Mwenyekiti wa ujumbe huo, Mohamed Chande Othman akisema, "Pande zinazopigana Sudan zina wajibu wa kisheria kuwalinda raia, lakini zimeonesha kutojali kufanya hivyo.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limetangaza kwamba moja ya magari yake jana yakisubiri kuingia kaskazini mwa Gaza lilishambuliwa kwa risasi za moto. Pia UNICEF imechapisha katika ukurasa wake wa mtandao wa X video ya Msemaji wa

  • Jifunze Kiswahili: Pata uchambuzi wa neno “PAMBAJIO”

    11/04/2024 Duration: 01min

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili  leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania , BAKITA anafafanua maana ya neno “PAMBAJIO”.

  • Alice Nderitu: Dunia bado haijajifunza lolote kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda dhidi ya Watutsi

    09/04/2024 Duration: 06min

    Miaka 30 iliyopita mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda yaliyoishangaza, dunia yalitokea kuanzia Aprili 7 mwaka 1994 na kudumu kwa siku 100 zilioghubikwa na ukatili wa hali ya juu na mamilioni ya watu kufurushwa makwao. Tangu wakati huo Umoja wa Mataifa umekuwa mstari wa mbele kuchukua hatua kuhakikisha asilani jinamizi hilo halitokei tena popote pale duniani. Manusura wa mauaji hayo wanasemaje kuhusu kumbukumbu hii? Na je dunia imejifunza nini kutokana na mauaji hayo ya Rwanda taifa ambalo limeshafungua ukurasa mpya na kuyapa kisogo? Twende mjini Kigali ambako kumbukumbu kubwa imefanyika mwishoni mwa wiki na itaendelea kwa siku 100, shuhuda wetu ni Eugene Uwimana afisa mawasiliano wa ofisi ya mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Rwanda.

  • 09 APRILI 2024

    09/04/2024 Duration: 10min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka mjini Kigali ambako kumbukumbu ya mauaji ya kimbari imefanyika mwishoni mwa wiki na itaendelea kwa siku 100. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani tunakupeleka nchini Sudan Kusini.Baada ya huduma ya ulinzi wa amani kwa zaidi ya miaka 20 huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, walinda amani kutoka China, hii leo wameondoka kutoka kambi yao iliyoko nje kidogo ya mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini, Bukavu ambako walishiriki kwa kiasi kikubwa katika ujenzi wa miundombinu.Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Olga Sarrado Mur katika mkutano na waandishi wa habari leo mjini Geneva, Uswisi ameeleza kwamba vita nchini Sudan ikikaribia kutimiza mwaka mmoja kamili na ikiendelea kupamba moto, idadi ya Wasudan waliolazimika kukimbia sasa imepita watu milioni 8.5, huku milioni 1.8 kati yao wakiwa wamevuka mipaka ya nchi. Na kwa mujibu wa Ripo

  • Mariam Suleiman: Wanawake tuna ujuzi, tuna uweo na tunaweza

    08/04/2024 Duration: 02min

    Mwanamke akiwezeshwa anaweza, huo ndio umekuwa usemi wa Umoja wa Mataifa ukipigia chepuo wanawake kujumishwa katika kila Nyanja ya Maisha ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuchangia katika maendeleo ya jamii. Usemi huo unaungwa mkono na mwanamke mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambaye sasa anaishi Kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Kutana na Mariam Suleiman ambaye kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR anasema vita ilimfungisha virago Congo DRC hadi hapa kambini Kakuma, ingawa ilimvurugia amani yake haikumkatishia ndoto zake za kuendelea na ufundi wa kuchomelea vyuma na pia kuwa mkufunzi wa kazi hiyo.“Katika kuchomelea vyuma ninafurahia sana kufanyakazi kazi hiyo ninapokwenda kazini na kujikuta ni mwanamke peke yangu uwanjani na hivyo ninajivunia sana kwa sababu sio kazi rahisi kwenda hapo ukiwa mwanamke peke yako katikati ya wanaume 15. Hivyo ninajivunia sana kuwa mchomelea vyuma na mkufunzi wa kuchomelea na kutengeneza vyuma”Kwa Mariam ma

page 1 from 5