Habari Za Un

Informações:

Synopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodes

  • FAO: Baa la njaa lanyemelea Gaza

    18/03/2024 Duration: 02min

    Hali ya uhakika wa kupata chakula huko Gaza, ni tete na baa la njaa linanyemelea kwenye majimbo ya kaskazini mwa eneo hilo imesema ripoti mpya ya  hali ya chakula Gaza iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, likisema jawabu la kuondokana na hali hiyo ni amani. Rein Paulsen, Mkurugenzi wa Ofisi ya Masuala ya Dharura na Mnepo FAO akizungumza hii leo huko Roma, Italia wakati wa kutolewa kwa ripoti hiyo ya uchambuzi wa viwango vya uhakika wa kupata chakula au IPC kwa Ukanda wa Gaza, anasema takwimu zinajenga taswira ya hali ya kutia wasiwasi mkubwa. Na pindi tunapofikiria kuhusu Gaza Kaskazini, ambako hali ni mbaya zaidi, uchambuzi wa sasa  unatuonesha kuwa njaa ni dhahiri katika kipindi cha kuanzia sasa na Mei 2024.Hii ina maana tunapotazama mwelekeo wa takwimu za hali ya upatikanaji chakula na lishe tunaona hali ya kutisha. Kusini, hali nayo imezidi kuwa mbaya na huko tunashikilia makadirio yetu ya uwezekano wa baa la njaa.”Ripoti inaonesha kuwa mwendelezo wa uhasama umesambara

  • 18 MACHI 2024

    18/03/2024 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia baa la njaa unalowakumba waPalestina katika ukanda wa Gaza, na kesi zinazohusisha wanajeshi wa nchi ya Sudan Kusini. Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, na mashinani tunakupeleka nchini Kenya, kulikoni? Hali ya uhakika wa kupata chakula huko Gaza, ni tete na baa la njaa linanyemelea kwenye majimbo ya kaskazini mwa eneo hilo imesema ripoti mpya ya  hali ya chakula Gaza iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, likisema jawabu la kuondokana na hali hiyo ni amani.Timu kutoka Kurugenzi ya Haki na Sheria ya Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF) mwishoni mwa wiki kwa usaidizi wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), imehitimisha tathmini yake katika Kaunti ya Maridi jimboni Equatorial Magharibi kutathmini kesi zinazohusisha wanajeshi wa nchi hiyo. Assumpta Massoi wa Idhaa hii akizungumza na Khadija Mrisho, Afisa kutoka shirika la kiraia la kutetea haki ardhi kwa mwanamke LANDESA tawi la Tanzania yeye aki

  • Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wasaidia jeshi la Sudan Kusini kutathmini kesi dhidi ya askari

    18/03/2024 Duration: 01min

    Timu kutoka Kurugenzi ya Haki Sheria ya Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF) mwishoni mwa wiki kwa usaidizi wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), imehitimisha tathmini yake katika Kaunti ya Maridi jimboni Equatorial Magharibi kutathmini kesi zinazohusisha wanajeshi wa nchi hiyo.Tathimini itawezesha kufunguliwa mashtaka kwa askari wa jeshi ambao wanashukiwa kufanya uhalifu mkubwa, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kingono na aina nyingine za unyanyasaji wa kijinsia.Mama Sarah Bennert, mwanaharakati na mwakilishi wa wanawake anasema hatua hii inawakilisha ishara ya haki na uwajibikaji."Tuna masuala mengi yanayotukabili hapa kama wanawake. Wakati mwingine unaripoti kesi na haki imechelewa na unabaki kukata tamaa na bila msaada wowote. Sasa, kwa uwepo wa timu ya tathmini hapa chini tunatumai kesi hizo zote walizozizingatia zitasikilizwa kwa sababu baadhi yetu ambao bado tuna kesi tuna kiwewe."Idrissa Sylvaine ni Mshauri wa haki sheria wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan

  • Ushirkiano wa dhati waliotuonesha ulifanya wananchi waachane na mpango wa kuwapiga mawe MONUSCO- Chifu Makofi

    15/03/2024 Duration: 03min

    Hii leo huko jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kikosi cha 10 cha Tanzania (TANZBATT-10)  kilichoko kwenye brigedi ya mapigano (FIB) ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO imekabidhi majukumu kwa kikosi cha 11, TANZBATT-11, katika hafla iliyofanyika eneo la Beni-Mavivi. Msimulizi wetu ni Kapteni Abubakari Muna, Afisa Habari wa TANZBATT-10.Mkuu wa TANZBATT-10 Luteni Kanali John Peter Kalabaka amekabidhi bendera ya Tanzania kwa Kamanda wa TANZBATT-11 Luteni Kanali Vedasto Ernest Kikoti ikiwa ni ishara ya kuanza majukumu ya ulinzi wa amani, katika tukio ambalo mgeni rasmi alikuwa Kaimu Kamanda wa FIB-MONUSCO Kanali Alex Tamson Malenda.Akizungumza kwenye hafla hiyo Luteni Kanali Kalabaka amesema kwenye upande wa operesheni wameweza kukabili na kupunguza mashambulizi yanayofanywa na vikundi vilivyojihami kwenye eneo la ulinzi la TANZBATT-10 halikadhalika kuepusha mauaji ya raia wasio na hatia na pia kuepusha vitendo vya ubakaji.“Kijamii tumeweza

  • Wasichana ni majaji watarajiwa, wafuate ndoto zao katika masomo ya Uanasheria - Hakimu Pamela Achieng

    15/03/2024 Duration: 06min

    Maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Majaji Wanawake duniani yalifanyika tarehe 10 Machi 2022, ikiangazia Haki katika Mtazamo wa Kijinsia.  Umoja wa Mataifa umeendelea kuadhimisha siku hii kama sehemu ya juhudi za kimataifa za kuhakikisha usawa wa kijinsia na kushughulikia masuala ya uadilifu wa mahakama yanayohusiana na jinsia. Huku mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68 ukiendelea hapa jijini New York Marekani, nchini Kenya Selina Jerobon wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kupitia video iliyoandaliwa na washirika wetu Redio Domus amekutana na Pamela Achieng, Hakimu katika mahakama ya Ngong iliyo katika Kaunti ya Kajiado ambaye anaanza kwa kuelezea ni kwa nini kama mwanamke aliamua kuingia katika tasnia hii.

  • 15 MACHI 2024

    15/03/2024 Duration: 12min

    Hii leo jaridani tunaangazia Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa ulinzi wa amani DRC, MONUSCO, na yaliyojiri katika mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani, CSW68. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?Hii leo huko jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kikosi cha 10 cha Tanzania (TANZBATT-10) kilichoko kwenye brigedi ya mapigano (FIB) ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO imekabidhi majukumu kwa kikosi cha 11, TANZBATT-11, katika hafla iliyofanyika eneo la Beni-Mavivi. Msimulizi wetu ni Kapteni Abubakari Muna, Afisa Habari wa TANZBATT-10.Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani, CSW68 ukiwa umeingia siku yake ya 5 leo, Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imekuwa ikizungumza na washiriki kutoka mataifa mbalimbali. Leo ni baadhi ya washiriki kutoka Tanzania, vinara wa elimu wanaofadhiliwa na Mfuko wa Malala. Katika makala ambapo hivi majuzi kuliadhimish

  • CSW68: Vinara wa elimu kutoka Tanzania wajizatiti kuhakikisha sauti za wasichana zinasikika

    15/03/2024 Duration: 02min

    Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani, CSW68 ukiwa umeingia siku yake ya 5 leo, Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imekuwa ikizungumza na washiriki kutoka mataifa mbalimbali. Leo ni baadhi ya washiriki kutoka Tanzania, vinara wa elimu wanaofadhiliwa na Mfuko wa Malala.Zahra Salehe Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali linaloitwa ICCAO anaeleza ujumbe mkubwa waliokuja nao.“Tumeletwa hapa kwa ajenda moja ya elimu na ujumbe mkubwa tuliokuja nao ni wa kuhakikisha sauti za wasichana na wanawake vijana zinasikika kwenye majukwaa makubwa kama haya CSW68 na sisi ajenda kubwa ambayo tunaiona kwas asa ni ‘reentry’ ambayo ni ruhusa ya msichana kurudi shule baada kupitia changamoto kubwa. Tisimuache mtu nyuma kwa sababu ya sababu mbalimbali ambazo zote zimeletwa na kutokuwa na usawa wa kijinsia. Wanaendelea na wanaendelea kutimiza ndoto zao.”Paulina Ngurumwa kutoka taasisi ya KINNAPA anakubaliana na anachosema kinara wa elimu mwenzake na anasema wanapambana na vikwazo dhidi ya elimu ya wanaw

  • Je wafahamu maana ya neno "Kupwemka?"

    14/03/2024 Duration: 01min

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua maana ya neno  “KUPWEMKA”.

  • 14 MACHI 2024

    14/03/2024 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, ambapo Jumuiya ya Madola anaelezea kinagaubaga mambo ambayo wanapenda kuona yanatekelezwa ili maudhui ya mwaka huu ya CSW68 ya kuwezesha wanawake kiuchumi na hatimaye kutokomeza umaskini yanafanikiwa. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za Haiti, Gaza na dawa za kulevya. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunakuletea uchambuzi wa neno “KUPWEMKA”Baada ya Kenya kutangaza kusitisha mpango wake wa kupeleka askari wa kuleta utulivu nchini Haiti hadi pale hali ya kisiasa itakapotengamaa, Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa Jumuiya ya kimataifa kusaidiana katika kuunda operesheni ya usaidizi kwa watu wa Haiti haraka iwezekanavyo.Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu dawa za kulevya (CND), imeanza mkutano wake hii leo huko Vienna Austria kukagua maendeleo yaliyopatikana katika kushughulikia tatizo la dawa za kulevya duniani na jinsi ya kuhakikisha utekelezaji wa ahadi za kimataifa. Na kukiwa na ripoti za kwamba leo Wapalestina 6 wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine 83

  • Kauli ya ‘usifanye hiki usifanye kile’ inadidimiza ndoto za wasichana – Frida Amani

    13/03/2024 Duration: 03min

    Makala hii inakupeleka Nairobi, Kenya ambako Priscilla Lecomte wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Mratibu wa hatua dhidi ya majanga ya tabianchi na El Niño anazungumza na Mwanamuziki Frida Amani wa Tanzania. Frida Amani anatoa wito kwa watoto wa kike duniani kutokatishwa tamaa kwa kuambiwa “usifanye shughuli fulani kwa kuwa ni ya kiume” kwani kama yeye angekata tamaa asingeweza kuwa msanii wa Hip Hop ambayo imemfikisha katika majukwaa ya kimataifa kiasi cha kuandaa wimbo wa kuhamasisha ushirikiano wa kimataifa katika kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, wimbo ambao umeungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira Duniani (UNEP). Hapa Frida anaanza kwa kueleza kwa nini wimbo alioshirikiana na msanii Dex Mc Bean wa Marekani waliamua kuupa jina Twende na Mpango.

  • Watoto waliouawa Gaza ni wengi kuliko miaka 4 ya vita duniani

    13/03/2024 Duration: 02min

    Wakati kukiwa na ripoti za mashambulizi kwa njia ya anga yanayotekelezwa na Israel huko Gaza usiku wa kuamkia leo, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA limesema idadi ya watoto waliouawa katika miezi ya hivi karibuni ni kubwa kuliko miaka minne ya mizozo duniani. Phillipe Lazzarini ambaye ni Mkuu wa shirika hilo la msaada kwa wakimbizi wa kipalestina hii leo kupitia mtandao wake wa X zamani Twitter ameandika ujumbe alioambatanisha na mchoro unaoonesha mambo mamwili kushoto kwenye rangi ya buluu idadi ya watoto waliouawa kutokana na vita tangu mwaka 2019 mpaka 2022 ambao ni 12, 193 na kulia ni idadi ya watoto waliouawa Gaza tangu mwezi Oktoba mwaka jana 2023 mpaka mwezi Februari 2024 ambao ni zaidi ya 12,300. Na ndipo akaandika ujumbe kuwa “Vita hii ni vita dhidi ya watoto. Ni vita dhidi ya utoto wao na mustakabali wao.”Mkuu huyo wa UNRWA akaendelea na ujumbe wake na kusema kuwa “Sitisheni mapigano sasa kwa ajili ya watoto wa Gaza“.Kwa mujibu wa takwimu kutoka mamlaka za afya

  • 13 JANUARY 2024

    13/03/2024 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia machafuko Gaza na afya ya watoto chini ya umri wa miaka 5. Makala tunakupeleka nchini Kenya na Mashinani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?Wakati kukiwa na ripoti za mashambulizi kwa njia ya anga yanayotekelezwa na Israel huko Gaza usiku wa kuamkia leo, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA limesema idadi ya watoto waliouawa katika miezi ya hivi karibuni ni kubwa kuliko miaka minne ya mizozo duniani kote.Idadi ya vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 duniani kote imepungua na kufikia kiwango cha chini zaidi kuwahi kufikiwa katika historia, ambapo takwimu mpya zilizotolewa na Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa mwaka 2022 idadi ya vifo ilikuwa chini ya milioni 4.9, sawa na pungufu kwa asilimia 51 tangu mwaka 2000. Makala inatupeleka Nairobi, Kenya ambako Priscilla Lecomte wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Mratibu wa hatua dhidi ya majanga ya tabianchi na El Niño anazungumza na Mwanamuziki Frida Amani wa Tanzania. Frida Amani anato

  • Juhudi za mashirika zafanikisha kupunguza vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka 5

    13/03/2024 Duration: 02min

    Idadi ya vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 duniani kote imepungua na kufikia kiwango cha chini zaidi kuwahi kufikiwa katika historia, ambapo takwimu mpya zilizotolewa na Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa mwaka 2022 idadi ya vifo ilikuwa chini ya milioni 4.9, sawa na pungufu kwa asilimia 51 tangu mwaka 2000. Ama hakika ni mafanikio makubwa kwani video iliyoambatana na habari hizi njema inaonesha madaktari, wakunga, wahudumu wa afya wakiwemo wale wa kijamii huko, Afrika, wakijituma kwa dhati kutoa huduma kuanzia kwa wajawazito, huduma za mama na mtoto hadi chanjo.Mathalani Sierra Leone anaonekana mhudumu wa afya akifika moja ya kaya kutoa huduma ya chanjo dhidi  ya Numonia au vichomi.Cambodia, Malawi, Mongolia na Rwanda zimetajwa kuwa ni nchi ambamo idadi ya vifo vya watoto hao imepungua kwa zaidi ya asilimia 75 kati ya 2000 na 2022.Ripoti imetolewa na kundi la mashirika na taasisi ya Umoja wa Mataifa, IGME, linaloongozwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambalo Mkurugenzi Mt

  • 12 MACHI 2024

    12/03/2024 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini India ambapo wahandisi wa usanifu majengo waliodhamiria kujenga mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kupunguza changamoto ya hewa ukaa katika sekta ya ujenzi kwa kutumia matofali ya matope. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani kama zifuatazo. Meli iliyosheheni misaada ya kibinadamu imeanza safari yake kutoka Cyprus kuelekea Gaza ikiwa na shehena ya tani 200 za misaada ya kuokoa maisha kwa ajili ya wananchi wa Gaza.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP hii leo linaonya kuwa litalazimika kusitisha misaada ya kuokoa maisha nchini Chad ifikapo mwezi ujao wa Aprili iwapo litakosa ufadhili wa haraka kwa ajili ya kusaidia wakimbizi. Na mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68, ukiendelea hapa jijini New York Marekani hii leo kutakuwa na mikutano ya kujadili mambo mbalimbali ikiwemo hali ya wanawake nchini Afghanistan, kuziba pengo la kujinsia kwenye elimu, athari za umaskini na uhalifu katika hud

  • Mlo shuleni umeongeza idadi ya wanafunzi wangu shule ya Salama: Mwalimu Beatrice Nyakoa Osaka

    11/03/2024 Duration: 06min

    Shule ya Salama iliyo katika eneo la Huruma karibu na mtaa wa mabanda wa Mathare jijini Nairobi Kenya hivi karibuni imeanza programu ya mlo shuleni kupitia mradi wa kampuni ya ‘Food for Education”. Hatua hiyo imenfa idadi ya wanafunzi wanaosoma shule hiyo kuongezeka kutoka 1, 900 hadi 2,300. Mlo shuleni ni moja ya masuala ambayo yanapigiwa debe kubwa na Umoja wa Mataifa sio tu kwa sababu ya kuhakikisha lishe bora kwa mamia ya maelfu ya wanafunzi ambao wengi hawawezi kupata mlo nyumbani bali pia kuongeza idadi ya watoto wanaohudhuria masomo. Stella Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Kenya UNIS Nairobi amefunga safari hadi shuleni Salama na kuzungumza na mwalimu mkuu wa shule hiyo Beatrice Nyakoa Osaka anayeenza kwa kufafanua umuhimu wa mradi huo shuleni kwake hasa kutokana na eneo walipo.

  • Mashambulizi na umwagaji damu vinaendelea Gaza licha ya kuanza kwa Ramadhan mauaji - Guterres

    11/03/2024 Duration: 02min

    Leo ni mwanzo wa mwezi mktukufu wa Ramadhan ambapo Waislamu kote duniani husherehekea na kuchagiza tunu za amani, maridhiano na mshikamano lakini uhasama unaendelea hususani sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Gaza ambako mauaji , na mashambulizi hayajakoma amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani hii leo. Hivyo ndivyo alivyoanza Katibu Mkuu katika tarifa yake fupi kwa waandishi wa habari akikumbusha kuwa ni hivi majuzi tuliingia mwezi wa sita tangu shambulio la kigaidi la Hamas nchini Israel na mashambulizi mabaya ya Israel huko Gaza. Ameo leo ana ombi kubwa ambalo ni “kuheshimu dhamira ya Ramadhani kwa kunyamazisha mtutu wa bunduki na kuondoa vikwazo vyote ili kuhakikisha utoaji wa misaada ya kuokoa maisha kwa kasi na kiwango kikubwa kinachohitajika.”Pia ametaka wakati huohuo kwa kuzingatia dhamira ya Ramadhani kuwaachilia mateka wote wanaoshikiliwa mara moja. Katibu Mkuu ameonya kwamba “Macho yadunia yanatazama. Macho ya historia yana

  • Mlo shuleni umeongeza idadi ya wanafunzi wangu shule ya Salama: Mwalimu Beatrice Osaka

    11/03/2024 Duration: 05min

    Shule ya Salama iliyo katika eneo la Huruma karibu na mtaa wa mabanda wa Mathare jijini Nairobi Kenya hivi karibuni imeanza programu ya mlo shuleni kupitia mradi wa kampuni ya ‘Food for Education”. Hatua hiyo imenfa idadi ya wanafunzi wanaosoma shule hiyo kuongezeka kutoka 1, 900 hadi 2,300. Mlo shuleni ni moja ya masuala ambayo yanapigiwa debe kubwa na Umoja wa Mataifa sio tu kwa sababu ya kuhakikisha lishe bora kwa mamia ya maelfu ya wanafunzi ambao wengi hawawezi kupata mlo nyumbani bali pia kuongeza idadi ya watoto wanaohudhuria masomo. Stella Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Kenya UNIS Nairobi amefunga safari hadi shuleni Salama na kuzungumza na mwalimu mkuu wa shule hiyo Beatrice Nyakoa Osaka anayeenza kwa kufafanua umuhimu wa mradi huo shuleni kwake hasa kutokana na eneo walipo

  • 11 MACHI 2024

    11/03/2024 Duration: 13min

    Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu kuhusu mwezi mktukufu wa Ramadhan, na uwezeshaji wa wanawake wakulima nchini Malawai. Makala na mashinani tunakupeleka nchini Kenya, kulikoni? Leo ni mwanzo wa mwezi mktukufu wa Ramadhan ambapo Waislamu kote duniani husherehekea na kuchagiza tunu za amani, maridhiano na mshikamano lakini uhasama unaendelea hususani sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Gaza ambako mauaji , na mashambulizi hayajakoma amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani hii leo.Nchini Malawi Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya Kilimo IFAD unatekeleza mradi wa kuwasaidia wanawake wa vijijini kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia na sasa wananachi wanafaidi matunda yake. Makala inatupeleka katika shule ya Salama iliyo katika eneo la Huruma karibu na mtaa wa mabanda wa Mathare jijini Nairobi Kenya hivi karibuni imeanza programu ya mlo shuleni kupitia mradi wa kampuni ya ‘Food for Education”. Hatua hiyo imenfa i

  • IFAD: Mradi wa ukulima nchini Malawi waboresha maisha ya na usawa kijinsia katika jamii

    11/03/2024 Duration: 02min

    Nchini Malawi Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya Kilimo IFAD unatekeleza mradi wa kuwasaidia wanawake wa vijijini kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia na sasa wananachi wanafaidi matunda yake. Mradi huo uitwao TRADE ulioanzishwa mwaka 2022 na serikali ya Malawi kwa kushirikiana na IFAD inalenga kubadilisha kilimo kupitia mpango wake wa Mseto na Ujasiriamali. Amos Mailosi ni Afisa Mazingira wa kanda Mabadiliko ya Tabianchi wa mradi huo wa TRADE na anasema jambo muhimu katika mradi wao ni kuhakikisha familia zinafanya kazi na kufikia maamuzi pamoja. “Moja ya eneo muhimu katika programu yetu ya TRADE ni kuhamasisha suala la ushirikishwaji wa kijinsia ndani ya jamii. Kwa hivyo, tunajaribu kuwawezesha wanawake na wanaume, na wavulana na wasichana, kushiriki kwa usawa katika afua. Ili kwa pamoja waweze kutambua umuhimu wa kufanya maamuzi ya pamoja katika ngazi ya kaya.”Kwa miaka mwili sasa mafanikio yameanza kuoneskana, na mmoja wa wanufaika hao ni Alefu Ofesa na mume wake Lloyd ambao wamekuwa wakulim

  • KIGOMa: Mafunzo ya kilimo hifadhi kutoka FAO chaongeza mavuno mahindi kutoka magunia 4 hadi 45

    08/03/2024 Duration: 03min

    Sasa ni makala inayotupeleka mkoani Kigoma, kaskazini-magharibi mwa Tanzania ambako huko shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limetekeleza kwa vitendo ujumbe wa mwaka huu wa siku ya wanawake duniani, Wekeza kwa Wanawake, Songesha Maendeleo, kwa kuwapatia mafunzo ya ufugaji bora wa kuku na mbuzi, halikadhalika kilimo hifadhi kisichoharibu mazingira. Sasa manufaa yako dhahiri kwani wanawake wameinuka kiuchumi. Miongoni mwao ni Hadija Alisido, mkazi wa kijiji Muhange, wilaya ya Kakonko. Katika makala hii inayoletwa kwako na Assumpta Massoi wa Idhaa hii, Hadija anaelezea alivyoinuliwa na FAO.

page 5 from 5