Habari Za Un

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 8:43:49
  • More information

Informações:

Synopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodes

  • Guterres: Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji tujikumbushe changamoto wanazokumbana nazo

    18/12/2024 Duration: 01min

    Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya Uhamiaji, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake mahususi kwa ajili ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji ametoa wito kwa ulimwengu kuitumia siku hii kujikumbusha kwamba pamoja na kwamba tunasherehekea michango ambayo mamilioni ya wahamiaji hutoa kwa jamii leo pia ni siku ya kujikumbusha changamoto ambazo wahamiaji wanaweza kukumbana nazo. Selina Jerobon na maelezo zaidi.

  • 18 DESEMBA 2024

    18/12/2024 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia siku ya wahamiaji duniani ikimulika mchango wa wakimbizi na wahamiaji katika ukuaji wa kiuchumi na kukuza jamii zao n aza wenyeji. Tutasikia kutoka mkuu wa IOM, Katibu Mkuu wa UN na wahamiaji Burundi na Chad. Pia tunaangazia ufugaji nyuki Tanzania.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake mahususi kwa ajili ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji ametoa wito kwa ulimwengu kuitumia siku hii kujikumbusha kwamba pamoja na kwamba tunasherehekea michango ambayo mamilioni ya wahamiaji hutoa kwa jamii leo pia ni siku ya kujikumbusha changamoto ambazo wahamiaji wanaweza kukumbana nazo.Nimefurahi sana kwani binti yangu mwenye ulemavu ambaye tulihamia naye makazi ya muda kufuatia kuongezeka kina cha maji ya Ziwa Tanganyika, hapa Burundi sasa amepatiwa stadi za kumwezesha kujikwamua kiuchumi. Ni kauli ya Odette Niyonkuru, raia mhamiaji wa ndani nchini Burundi akizungumzia mustakabali wa binti yake huyo kwenye video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM.Makala i

  • Mafunzo ya IOM kwa msichana mhamiaji mwenye ulemavu, yaleta furaha kwa mama yake

    18/12/2024 Duration: 02min

    Nimefurahi sana kwani binti yangu mwenye ulemavu ambaye tulihamia naye makazi ya muda kufuatia kuongezeka kina cha maji ya Ziwa Tanganyika, hapa Burundi sasa amepatiwa stadi za kumwezesha kujikwamua kiuchumi. Ni kauli ya Odette Niyonkuru, raia mhamiaji wa ndani nchini Burundi akizungumzia mustakabali wa binti yake huyo kwenye video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM. Odette anaenelea kueleza manufaa ya uwezeshaji huu kwa bintiye kama anavyofuatilia Assumpta Massoi.

  • 17 DESEMBA 2024

    17/12/2024 Duration: 10min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika mafanikio katika kuzuia maambukizi mapya ya VVU na juhudi za vijana wakimbizi nchini Uganda kuhakikisha hilo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani inayotupeleka Gaza.Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Geir O. Pedersen bado yuko nchini Syria alikowasili jana Jumapili  ikiwa ni wiki moja baada ya wapiganaji wa Hayʼat Tahrir al-Sham (HTS) walioko kwenye orodha ya vikundi vya kigaidi kutwaa mji mkuu Damascus na kusababisha Rais Bashar Al-Assad kukimbia nchi.Mwaka 2024 ukielekea ukingoni, sirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Uganda limetoa rai kwa jumiya ya kimataifa kutolisahau taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo ni maskani ya idadi kubwa zaidi ya waomba hifadhi na wakimbizi barani Afrika. Rai hiyo iliyotolewamwishoni mwa wiki inataka ufadhili wa fedha uongezwe ili liweze kuendelea kukirimu watu hao ambao wengi wanakimbia machafuko.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,

  • Harakati za wazazi kuona watoto wao wanasajiliwa nchini mwao baada ya kuzaliwa

    16/12/2024 Duration: 04min

    Tarehe 11 mwezi huu wa Desemba, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF lilitoa ripoti yake kuhusu usajili wa vizazi duniani ikionesha maendeleo makubwa katika idadi ya watoto wanaosajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa. Maeneo mengine kama nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara ongezeko ni dogo ikilinganishwa na kwingineko. Ingawa hivyo licha ya changamoto zilizoko kwa nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara katika kutoa huduma hiyo, mafanikio yanaanza kuonekana kama inavyosimulia makala hii iliyoandaliwa na Assumpta Massoi kupitia video ya UNICEF.

  • Mjumbe wa UN aendelea na ziara ya kukutana na wadau nchini Syria

    16/12/2024 Duration: 01min

    Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Geir O. Pedersen bado yuko nchini Syria alikowasili jana Jumapili  ikiwa ni wiki moja baada ya wapiganaji wa Hayʼat Tahrir al-Sham (HTS) walioko kwenye orodha ya vikundi vya kigaidi kutwaa mji mkuu Damascus na kusababisha Rais Bashar Al-Assad kukimbia nchi. Ikiwa ni sehemu ya juhudi za Umoja wa Mataifa kuhakikisha mabadiliko ya utawala nchini Syria yanafanyika kwa amani na kuisaidia Syria kutokuingia kwenye mgogoro zaidi, Bwana Pederson aliyewasili jana Damascus  hadi sasa ameshakutana na Kamanda wa Utawala Mpya Ahmed al-Sharaa na Waziri Mkuu wa Serikali ya Muda Mohammed al-Bashir.Taarifa iliyotolewa leo na Ofisi yake inasema Pederson ameeleza muhtasari wa matokeo ya Mkutano wa Kimataifa wa Aqaba kuhusu Syria uliofanyika tarehe 14 ya mwezi huu wa Desemba akisisitiza haja ya kuwepo kwa mpito wa kisiasa unaoaminika na unaoongozwa na kumilikiwa na Wasyria wenyewe kama kanuni za azimio 2254 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (2015) zilivyopendekeza.

  • 16 DESEMBA 2024

    16/12/2024 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia serikali ya mpito nchini Syria na wakimbizi na wahamiaji wanaosaka hifadhi nchini Uganda. Makala tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Geir O. Pedersen bado yuko nchini Syria alikowasili jana Jumapili  ikiwa ni wiki moja baada ya wapiganaji wa Hayʼat Tahrir al-Sham (HTS) walioko kwenye orodha ya vikundi vya kigaidi kutwaa mji mkuu Damascus na kusababisha Rais Bashar Al-Assad kukimbia nchi.Mwaka 2024 ukielekea ukingoni, sirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Uganda limetoa rai kwa jumiya ya kimataifa kutolisahau taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo ni maskani ya idadi kubwa zaidi ya waomba hifadhi na wakimbizi barani Afrika. Rai hiyo iliyotolewamwishoni mwa wiki inataka ufadhili wa fedha uongezwe ili liweze kuendelea kukirimu watu hao ambao wengi wanakimbia machafuko.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Et

  • UNHCR: Chonde chonde jumuiya ya Kimataifa tuishike mkono Uganda kwa faida ya waomba hifadhi na wakimbizi

    16/12/2024 Duration: 02min

    Mwaka 2024 ukielekea ukingoni, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR  nchini Uganda limetoa rai kwa jumuiya ya kimataifa kutolisahau taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo ni maskani ya idadi kubwa zaidi ya waomba hifadhi na wakimbizi barani Afrika. Rai hiyo iliyotolewa mwishoni mwa wiki inataka ufadhili wa fedha uongezwe ili liweze kuendelea kukirimu watu hao ambao wengi wanakimbia machafuko. Huyo ni Moulid Hujale afisa wa UNHCR nchini Uganda akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kushikamana na Uganda akiwa  kwenye makazi makubwa ya wakimbizi ya Kiryandongo Magharibi mwa nchi hiyo. Anasema kuna mambo matatu muhimu ambayo dunia inapaswa kufahamu kuhusu Uganda na wakimbizi.“Mosi Uganda inahifadhi idadi kubwa zaidi ya wakimbizi na waomba hifadhi Afrika ikiwa na zaidi ya watu milioni 1.7 wengi wao wakitoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Sudan Kusini.”Zaidi ya hapo ukarimu wa Uganda anasema hauna kipimo“Pili, Uganda ina sera ya kufugua mlango kwa wakimbizi na pia kwa miong

  • Sasa tunalima mboga shuleni na nyumbani - Wanafunzi Buhigwe Tanzania

    13/12/2024 Duration: 03min

    Kupitia mradi wa Pamoja wa Kigoma, KJP,  awamu ya Pili, Shule ya Msingi Buhigwe, iliyoko wilayani Buhigwe, mkoa wa Kigoma, ilipatiwa mafunzo kupitia Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), likishirikiana na asasi isiyo ya kiserikali RECODA. Mafunzo haya yalilenga mbinu bora za kilimo ambapo wanafunzi waliweza kuanzisha bustani za mboga kupitia somo la Elimu ya Kujitegemea. Mradi umeanza kutekelezwa na matunda yanaanza kuonekana kama asimuliavyo Assumpta Massoi kwenye makala hii.

  • UNFPA yasambaza huduma muhimu ya ukunga kwa wakimbizi wa Sudan nchini Chad

    13/12/2024 Duration: 01min

    Kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi wanaoingia Chad wakitoka Sudan kuwa ni wanawake na watoto, Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi,  UNFPA limeimarisha huduma za afya ya wanawake na watoto kama anavyosimulia Selina Jerobon.

  • 13 DESEMBA 2024

    13/12/2024 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia hali nchini Syria, na msaada wa kibinadamu kw awakimbizi nchini Chad. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, kulikoni?Ofisi ya mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria (OSE) imesema wakati huu ikifuatilia kwa karibu hali na maendeleo nchini Syria ni muhimu kuhakikisha kwamba Wasyria wanashika usukani wa mustakbali wao na kwamba kuna ujumbe wa pamoja na mshikamono kuhusu hilo kutoka kwenye jumuiya ya kimataifa.Kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi wanaoingia Chad wakitoka Sudan kuwa ni wanawake na watoto, Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi,  UNFPA limeimarisha huduma za afya ya wanawake na watoto.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Tanzania kusikia jinsi wanafunzi wananufaika na mradi wa Umoja wa Mataifa shuleni na majumbani.Na mashinani fursa ni yake Aline kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC ambaye ni mnufaika wa mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula

  • UN: Lazima kuhakikisha Wasyria wanashika usukani wa mustakbali wao

    13/12/2024 Duration: 01min

    Ofisi ya mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria (OSE) imesema wakati huu ikifuatilia kwa karibu hali na maendeleo nchini Syria ni muhimu kuhakikisha kwamba Wasyria wanashika usukani wa mustakbali wao na kwamba kuna ujumbe wa pamoja na mshikamono kuhusu hilo kutoka kwenye jumuiya ya kimataifa. Flora Nducha na taarifa zaidi.

  • Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi maana ya neno MIDABWADA

    12/12/2024 Duration: 28s

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno MIDABWADA” 

  • 12 DESEMBA 2024

    12/12/2024 Duration: 10min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa ikiangazia wanawake na wasichana mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ambapo ukatili wa kingono ni jinamizi linalowakumba kila uchao kutokana na mapigano yanayoendelea kwenye eneo hilo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno MIDABWADA.Leo si siku ya kimataifa ya huduma za afya kwa wote mwaka huu ikibeba mudhui “Huduma za afya kwa wote ni jukumu la serikali” yakisisitiza kwamba Uwekezaji katika huduma za afya kwa wote UHC, unaimarisha usawa na uwiano wa kijamii na pia unanufaisha uchumi wa taifa kwa kuboresha afya na ustawi, kuongeza ushiriki wa wafanyikazi na tija, na kujenga mnepo kwa watu, familia na jamii.Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syri Geir O. Pedersen leo amesema “Picha kutoka kwenye magereza ya Sednaya na vituo vingine vya kizuizini nchini Syria vinadhihirisha unyama na ukatili usiofikirika ambao Wasyria wamevumilia na umekuwa ukiripotiwa kwa miaka mingi.”Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres yuko z

  • Baada ya kunusuriwa na programu ya IOM, mhamiaji kutoka nchini Ethiopia asema katu hatorudi Yemen

    11/12/2024 Duration: 04min

    Janga la kibinadamu likizidi kushika kasi nchini Yemen, shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM linaongeza kasi ya mpango wake wa kurejesha wahamiaji nyumbani kwa hiari, VHR. Mradi huu hupatia wahamiaji waliokwama njia salama ya kurejea nyumbani kwao. Kupanuliwa kwa mradi huu kunafuatia idadi ya wahamiaji nchini Yemen kuongezeka na kufikia 6,300 mwezi Oktoba mwaka huu, kwa mujibu wa mfuko wa IOM wa  Ufuatiliaji wa wahamiaji.Mwaka huu wa 2024, IOM imeshafanya safari 30 za ndege kupitia mradi huo wa VHR ikiwemo ya tarehe 5 mwezi huu waDesemba ambapo wahamiaji 175 wa Ethiopia walirejeshwa Yemen kutoka uwanja wa ndege wa Aden. Makala hii inafuatilia miongoni mwa wahamiaji hao yaliyowasibu hadi kukubali kurejea nyumbani kwa hiari. Msimulizi wako ni Assumpta Massoi.

  • UNICEF nchini Rwanda kwa kushirikiana na UNICEF Switzerland na Liechtenstein wafanikisha ‘kinesitherapy’ kwa watoto

    11/12/2024 Duration: 01min

    Nchini Rwanda Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa msaada wa UNICEF Switzerland na Liechtenstein wamesaidia tiba kwa njia ya mazoezi kuponya watoto wenye ulemavu wa viungo. Selina Jerobon anasimulia akiangazia mtoto mmoja, Joshua.

  • 11 DESEMBA 2024

    11/12/2024 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya WHO inayohusu malaria, na juhudi za UNICEF na wadau wake nchini Rwanda za kusaidia watoto waliozaliwa na ulemavu kuweza kutembea. Makala tunakupeleka nchini Yemen na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Takwimu mpya zilizotolewa leo na ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO, zinaonyesha kuwa ingawa takriban wagonjwa bilioni 2.2 wa malaria na vifo milioni 12.7 vya ugonjwa huo vimeepukwa tangu mwaka 2000 bado ugonjwa huo unaendelea kuwa tishio kubwa la kimataifa la afya hususan katika Kanda ya Afrika ya WHO na hivyo juhudi zaidi zahitajika kuutokomeza.Nchini Rwanda Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa msaada wa UNICEF Uswisi na Liechtenstein wamesaidia tiba kwa njia ya mazoezi kuponya watoto wenye ulemavu wa viungo. Selina Jerobon anasimulia akiangazia mtoto mmoja, Joshua.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Yemen kusikia yaliyojiri baada ya ndoto za vijana kuelekea Saudi Arabia kuishia Yemen.Na mashinani mashinani hivi majuzi d

  • WHO: Ingawa vifo milioni 12.7 vya malaria vimeepukwa juhudi zaidi zahitajika kutokomeza gonjwa hilo

    11/12/2024 Duration: 01min

    Takwimu mpya zilizotolewa leo na ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO zinaonyesha kuwa ingawa takriban wagonjwa bilioni 2.2 wa malaria na vifo milioni 12.7 vya ugonjwa huo vimeepukwa tangu mwaka 2000 bado ugonjwa huo unaendelea kuwa tishio kubwa la kimataifa la afya hususan katika Kanda ya Afrika ya WHO. Taarifa ya Flora Nducha inafafanua zaidi.

  • UNFPA: Elimu ndio ufunguo wa kutokomeza FGM Kenya

    10/12/2024 Duration: 05min

    Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya haki za binadamu tunaelekea Kenya kuangazia moja ya ukiukwaji Mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya wanawake, jinamizi la ukeketaji na jitihada zinazochukuliwa na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa  ya idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA kutokomeza janga hilo. Mwandishi wetu wa Nairobi Thelma Mwadzaya amefuatilia kuhusu suala hilo na kwa undani zaidi ungana naye ..

  • 10 DESEMBA 2024

    10/12/2024 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na tunaelekea nchini Kenya kuangazia moja ya ukiukwaji Mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya wanawake, jinamizi la ukeketaji na jitihada zinazochukuliwa na UNFPA na wadau mbalimbali. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani inayotupeleka nchini Namibia.Baada ya serikali ya Bashar Al-Assad kupinduliwa na kuibuka kwa taarifa za baadhi ya nchi duniani kuanza kusitisha mchakato wa kushughulikia maombi ya Wasyria waliokuwa wameomba hifadhi kuokoa usalama wa maisha yao pindi hali ilipokuwa tete nchini mwao, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) linaendelea kutoa wito kwa mataifa yote kufungua milango, kuwapa hifadhi na ulinzi raia wa Syria wanaotafuta usalama. UNHCR imeahidi pia mara tu hali ya Syria itakapokuwa wazi zaidi, itatoa mwongozo kuhusu mahitaji ya ulinzi kwa Wasyria walioko hatarini.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limekaribisha mchango wa dola za Marekani milioni 22 kutoka shirika la Korea Kusini la Ushir

page 2 from 5