Synopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodes
-
31 DESEMBA 2024
31/12/2024 Duration: 12minKipindi maalumu wakimbizi, wakimbizi wa ndani na wenyeji wao wanaeleza namna walivyonufaika na misaada ya Umoja wa Mataifa na mashirika yake na pia wanaeleza matumaini yao kwa mwaka ujao wa 2025.
-
-
-
30 DESEMBA 2024
30/12/2024 Duration: 10minLeo jaridani: Mwaka 2024 ulighubikwa na machungu lakini kuna matumaini 2025 asema Guterres.UNMAS yaondolea hofu wakulima Beni, DRC kwa kutegua masalia ya mabomu.Makala inatupeleka Uganda kusikiliza msichana mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Ashiimwe Baganiza mwenye ndoto ya kuwa wakili ili kuwatetea wanawake.Mashinani ni mradi wa Siku 1000 wa UNICEF Zambia.
-
Nilikuwa miongoni mwa Wacuba wa kwanza kujifunza Kiswahili: Profesa Jacomino
27/12/2024 Duration: 05minUjumuishwasji wa lugha mbalimbali katika dunia iliyoshikamana katika Nyanja mbalimbali ni moja ya malengu ya Umoja wa Mataifa kuanzia katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa hadi kwenye nchi wanachama unalichagiza hilo. Hamasa hiyo imezichagiza nchi nyingi kuanza kukumbatia lugha ambazo kwa asili hazizungumzwi kama alivyobaini Flora Nducha wa Idhaa hii ambaye hivi karibuni alikuwa Cuba kwenye Kongamano la Kimataifa la Kiswahili na kukutana na Profesa Juan Jacomino ambaye ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Havana na ni miongoni mwa watu wa mwanzo waliokwenda Tanzania kujifunza Kiswahili na sasa anakifundisha nchini mwake Cuba. Anafafanua kuhusu safari yake ya kujua Kiswahili katika makala hii..
-
Siku ya Kimataifa ya Kujitayarisha dhidi ya magonjwa ya mlipuko, Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito
27/12/2024 Duration: 01minKatika kuandhimisha Siku ya Kimataifa ya Kujitayarisha dhidi ya Magonjwa ya Mlipuko, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito kwa nchi kote ulimwenguni kuzingatia masomo yaliyopatikana katika dharura za kiafya zilizopita ili kusaidia kujiandaa kwa dharura zijayo. Assumpta Massoi anaeleza zaidi.
-
27 DESEMBA 2024
27/12/2024 Duration: 09minHii leo jaridani tunaangazia sherehe za krismasi katika ukanda wa Gaza lich ya migogoro inayoendelea, na magonjwa ya mlipuko. Makala inatupeleka Havana Cuba na mashinani nchini Uganda, kulikoni?Katika kuandhimisha Siku ya Kimataifa ya Kujitayarisha dhidi ya Magonjwa ya Mlipuko, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito kwa nchi kote ulimwenguni kuzingatia masomo yaliyopatikana katika dharura za kiafya zilizopita ili kusaidia kujiandaa kwa dharura zijayo.Tukiwa bado katika msimu wa sikukuu ya krismasi, tunakwenda mji wa Gaza, huko Ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati kusikia jinsi sikukuu hii ilivyoadhimishwa na hisia mchanganyiko kwenye kanisa katoliki la Familia Takatifu kwenye viunga vya zamani kwenye mji huo.Makala inatupeleka Havana Cuba kuangazia umuhimu wa utekelezaji wa moja ya ajenda za Umoja wa Mataifa ya kukumbatia lugha mbalimbali duniani ambapo Flora Nducha wa Idhaa hii akiwa Cuba hivi karibuni kwenye kongamano la Kimataifa la Kiswalihi alikutana na raia wa nchi ambaye ni mwalimu w
-
Sherehe za Krismasi katika ukanda wa Gaza, wakimbizi wa ndani wataka vita vikome
27/12/2024 Duration: 02minTukiwa bado katika msimu wa sikukuu ya krismasi, tunakwenda mji wa Gaza, huko Ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati kusikia jinsi sikukuu hii ilivyoadhimishwa na hisia mchanganyiko kwenye kanisa katoliki la Familia Takatifu kwenye viunga vya zamani kwenye mji huo. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.
-
24 DESEMBA 2024
24/12/2024 Duration: 12minHii leo jaridani tunakuletea mad akwa kina inayotupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kumulika harakati za kusaidia manusura wa ukatili wa kingono na kijinsia kwenye mizozo. Pia tunakuletea muhtasari wa había za Sudan, Uganda na Tanzania, Mashinani tunarejea Sudan.Ripoti ya Kamati ya Tathmini ya Viwango vya Njaa (IPC) iliyotolewa leo inaeleza kwamba imegundua kuwa kuna maeneo matano zaidi nchini Sudan ambayo yanakabiliwa na baa la njaa kati ya mwezi huu wa Desemba na Mei mwaka ujao wa 2025. Ripoti hiyo imeyataja maeneo hayo kuwa ni ya Darfur Kaskazini yaani Um Kadadah, Melit, El Fasher, Twawisha, na Al Lait.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limekaribisha mchango wa EURO milioni 1 kutoka serikali ya Ujerumani ili kusaidia shughuli za lishe na ustawi kwa zaidi ya wakimbizi na wasaka hifadhi 254,000 nchini Uganda ambayo inawahifadhi wakimbizi milioni 1.7.Na Kikosi cha 7 cha Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, TANBAT 7 kilichokuwa kinahudumu katika Ujumbe wa Um
-
Mradi wa kilimo cha umwagiliaji warejesha matumaini kwa wakulima wa Masvingo, Zimbabwe
23/12/2024 Duration: 03minHivi karibuni mkutano wa Umoja wa Mataifa wa kuzuia kuenea kwa jangwa, ulikunja jamvi huko Riyadh, Saudi Arabia ambapo Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD ulitumia fursa hiyo kuelezea harakati zake za kusaidia wakulima barani Afrika walioathiriwa vibaya na kuenea kwa jangwa. Miongoni mwa mataifa hayo ni Zimbabwe ambako IFAD imeshaanza kuchukua hatua na kuleta nuru kwa wakulima kama anavyosimulia Assumpta Massoi kwenye makala hii.
-
Mkuu wa ofisi ya OCHA Tom Fletcher aeleza aliyoyashuhudia ziara yake ya kwanza Mashariki ya Kati
23/12/2024 Duration: 01minMkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Dharura, OCHA, Tom Fletcher akihitimisha ziara yake ya kwanza katika eneo la Mashariki ya kati tangu hivi karibuni alipochukua wadhifa huo ameeleza kuwa alichokishuhudia katika ukanda huo ni hali tete. Selina Jerobon anaeleza zaidi.
-
23 DESEMBA 2024
23/12/2024 Duration: 10minHii leo jaridani tunaangazia ziara ya Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Dharura, OCHA, Tom Fletcher mashariki wa kati, na uwezeshaji wa vijana katika sekta ya kilimo nchini humo. Makala inatupeleka nchini Zimbabwe na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Dharura, OCHA, Tom Fletcher akihitimisha ziara yake ya kwanza katika eneo la Mashariki ya kati tangu hivi karibuni alipochukua wadhifa huo ameeleza kuwa alichokishuhudia katika ukanda huo ni hali tete.Mradi wa pamoja wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO ujulikanao kama Nabta kwa lugha ya Kiarabu ukimaanisha "mche" ambao lengo lake ni kuwasaidia vijana wajasiriamali kubadili mawazo yao kuwa biashara ya kilimo yenye mafanikio umeleta nuru kwa Alaa Khattab kijana aliyekuwa na ndoto ya kuwa mfanyabiashara wa kilimo nchini Syria.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Zimbabwe kumulika nuru iliyofikia wakulima baada ya Umoja wa Mataifa kuona jinsi mabadiliko ya tabianc
-
Hadithi ya Alaa Khattab: Kutoka kuwa mzalishaji mdogo kijijini kwake hadi kuwa msafirishaji wa Kikanda wa achari
23/12/2024 Duration: 02minMradi wa pamoja wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO ujulikanao kama Nabta kwa lugha ya Kiarabu ukimaanisha "mche" ambao lengo lake ni kuwasaidia vijana wajasiriamali kubadili mawazo yao kuwa biashara ya kilimo yenye mafanikio umeleta nuru kwa Alaa Khattab kijana aliyekuwa na ndoto ya kuwa mfanyabiashara wa kilimo nchini Syria. Flora Nducha anatujuza zaidI.
-
Wasichana wakipewa fursa hakuna mchezo utakaowashinda: Saido Noor
20/12/2024 Duration: 03minKutana na Saido Omar Noor, binti mwenye umri wa miaka 25 mkimbizi kutoka Somalia anayeishi Kakuma kambi kubwa zaidi ya wakimbizi nchini Kenya. Kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR anasema katika jamii yake ni yeye mwanamke pekee wa Kisomali anayecheza mpira kwa kikapu au basketball. Flora Nducha na taarifa zaidi..
-
Rwanda yatangaza mwisho wa mlipuko wa Marburg, WHO yapongeza Rwanda
20/12/2024 Duration: 02minShirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limeipongeza serikali ya Rwanda kwa kufanikiwa kuudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Maburg. Hii leo Rwanda imetangaza mwisho wa mlipuko wa hivi karibuni wa ugonjwa huo baada ya kutokuwepo maambukizi mapya katika siku 42 na mgonjwa wa mwisho akiwa amepimwa mara mbili bila kukutwa na ugonjwa kama matakwa ya WHO yanavyotaka ili kutangaza kuisha kwa mlipuko wa magonjwa namna hii. Selina Jerobon na maelezo zaidi.
-
20 DESEMBA 2024
20/12/2024 Duration: 10minHii leo jaridani tunaangazia jitihada za kuudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Maburg nchini Rwanda, na juhudi za kuchunguza virusi vya VVU nchini Ghana. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini DRC, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limeipongeza serikali ya Rwanda kwa kufanikiwa kuudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Maburg. Hii leo Rwanda imetangaza mwisho wa mlipuko wa hivi karibuni wa ugonjwa huo baada ya kutokuwepo maambukizi mapya katika siku 42 na mgonjwa wa mwisho akiwa amepimwa mara mbili bila kukutwa na ugonjwa kama matakwa ya WHO yanavyotaka ili kutangaza kuisha kwa mlipuko wa magonjwa namna hii.Mwaka 2020 Ghana iliripoti kuwa na watu 350,000 wanaioshi na virusi vya Ukimwi na kati yao hao 31,000 walikuwa ni wajawazito. Jambo lililoshtua ni kwamba ni sehemu ndogo mno ya wajawazito hao ndio walipimwa kufahamu iwapo wana VVU au la. Jambo lililofanya serikali kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kuchukua hatua.Makala inatupeleka kwenye ka
-
Kipimo cha GeneXpert chaleta mapinduzi kwenye upimaji wa VVU nchini Ghana
20/12/2024 Duration: 02minMwaka 2020 Ghana iliripoti kuwa na watu 350,000 wanaioshi na virusi vya Ukimwi na kati yao hao 31,000 walikuwa ni wajawazito. Jambo lililoshtua ni kwamba ni sehemu ndogo mno ya wajawazito hao ndio walipimwa kufahamu iwapo wana VVU au la. Jambo lililofanya serikali kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kuchukua hatua. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi.
-
Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa neno Akraba
19/12/2024 Duration: 38sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya neno “AKRABA.”
-
19 DESEMBA 2024
19/12/2024 Duration: 09minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Syria, ambako viongozi wa ngazi mbalimbali za Umoja wa Mataifa wamendelea kusisitiza hitaji la kutanguliza ulinzi wa manusura na uhifadhi wa ushahidi wa uhalifu. Pia tunapata ufafanuzi wa neno na muhtasari wa habari.Karla Quintana kutoka Mexico ameteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres hii leo kuongoza Taasisi Huru ya kuchunguza watu waliotoweshwa nchini Syria, taasisi ambayo imeundwa na Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Juni mwaka jana 2023. Guterres amewaambia waandishi wa habari hii leo kwamba yeye na timu yake lazima waruhusiwe kutekeleza kwa kina jukumu lao, na vile vile mifumo yote ya kimataifa ya kusongesha ulinzi wa haki za binadamu nchini Syria na uwajibikaji wa uhalifu uliotendwa lazima wawe na wanachohitaji ili kutekeleza majukumu yao muhimu.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa na kikao cha ngazi ya mawaziri kuhusu Akili Mnemba, au AI ambapo Katibu Mkuu António Guterres amesema pamoja faida kub
-
FAO Tanzania yatoa mafunzo ya ufugaji wa nyuki kwa wenyeji Tanzania kupitia Mradi wa ACP MEAs 3
18/12/2024 Duration: 02minMradi wa ACP MEAs 3 unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO, na kufadhiliwa na Muungano wa Ulaya, EU umetoa mafunzo ya ufugaji nyuki kwa wakulima nchini Tanzania. Mradi huu unawapa wakulima zana na ujuzi muhimu katika ufugaji nyuki endelevu, na hivyo kuboresha maisha yao huku wakikuza bayoanuwai na uhifadhi wa mazingira. Kwa kuunga mkono jamii za wenyeji, Mradi huu unalenga kukuza ukuaji wa uchumi na kuwawezesha wakulima kulinda wachavushaji, ambao ni muhimu kwa uzalishaji katika kilimo na afya ya mfumo ikolojia. Tupate simulizi zaidi katika makala hii iliyoandaliwa na Flora Nducha kupitia video ya FAO Tanzania.