Gurudumu La Uchumi

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 2:59:59
  • More information

Informações:

Synopsis

Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .

Episodes

  • Akili unde na mustakabali wa uchumi wa Afrika: Fursa mpya kwa vijana wabunifu

    22/04/2026 Duration: 10min

    Katika kipindi ambacho Afrika inaendelea kukabiliana na changamoto za kiuchumi na kijamii, teknolojia ya Akili Unde (AI) inaibuka kama nyenzo muhimu ya kuleta mabadiliko. Kutoka kilimo hadi afya, na kutoka elimu hadi utawala bora, ubunifu wa kidijitali unaanza kubadilisha namna matatizo ya muda mrefu yanavyotatuliwa.Katika makala hii, tunazungumza na Kevin Obote kijana mbunifu wa teknolojia ambaye anatumia AI kuunda suluhisho zinazolenga mazingira halisi ya Afrika.

  • Kwa nini vikwazo vya usafirishaji ni kizuizi kikubwa cha biashara Afrika Mashariki

    01/04/2026 Duration: 09min

    Kupitia ripoti iliyozinduliwa juma hili na shirikisho la wazalishaji nchini Kenya, inaonyesha kuwa kusafirisha bidhaa katika njia muhimu za biashara za Afrika bado ni ghali na haitabiriki, ambapo wakati mwingine hugharimu hadi dola 7,000 za Marekani kwa kontena moja kati ya Nairobi na Lusaka. Kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, tumezungumza na Tobias Alando, mkurugenzi mtendaji wa shirikisho la wamiliki wa viwanda nchini Kenya.

  • Uwazi kwenye ubinafsishaji wa mashirika ya uma ni muhimu kwa maendeleo

    11/03/2026 Duration: 10min

    Msikilizaji Katika miaka ya hivi karibuni, nchi nyingi za Afrika Mashariki zimekuwa zikifanya mageuzi makubwa ya kiuchumi. Mojawapo ya mageuzi hayo ni ubinafsishaji wa mashirika ya umma. Leo tunajiuliza, Je, ubinafsishaji ni kweli unasaidia uchumi kukua, au serikali inapaswa kubaki na umiliki wa mashirika muhimu?

  • Vita ya Iran: Afrika imejipangaje kukabiliana na athari za kiuchumi

    04/03/2026 Duration: 10min

    Msikilizaji mara zote mgogoro wa mashariki ya kati, umekuwa na athari hasi za kiuchumi na biashara duniani, Swali kubwa tunajiuliza hivi leo ni Je, Afrika iko salama kiasi gani? Vita hivi vitaathiri vipi uchumi wa dunia — na gharama za maisha kwa mwananchi wa kawaida barani Afrika?

  • Ushirikishwaji wa wanawake katika sekta za kiuchumi chanzo cha ukuaji wa uchumi

    25/02/2026 Duration: 10min

    Benki ya Dunia inasema hata katika nchi zenye sheria za kisasa kuhusu usawa kazini, nchi hizo zimeshindwa kuzitekeleza, hadi sasa hakuna nchi iliyofikia kiwango cha juu cha usawa kazini, n ani asilimia kidogo tu ya wanawake wanaishi kwenye nchi zenye angalau sheria bora, huku mataifa 70 ikiwemo Misri, Madagascra na Somalia zikipiga hatua katika kuboresha mazingira ya usawa kati yam waka 2023 na 2025. 

  • Ushirikiano wa kikanda hatarini: Nakisi ya bajeti yaibua maswali mapya

    18/02/2026 Duration: 09min

    Juma hili tunajadili kuhusu mustakabali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, hasa wakati huu kukiwa na taarifa kuwa inakabiliwa na mgogoro wa kifedha. Taarifa zinaonesha kuwa Jumuiya hiyo inakabiliwa na upungufu wa bajeti unaofikia karibu dola za marekani milioni 89, pengo ambalo huenda likatatiza shughuli za Jumuiya hiyo, jambo ambalo limemfanya rais wa Kenya William Ruto ambaye ni mwenyekiti wa jumuiya kwa sasa, kuitisha mkutano wa dharura wa wakuu wan chi mwezi ujao.

  • Dubai: Viongozi wa dunia waangazia mageuzi ya sera, ubunifu na mifumo mipya ya utawala

    05/02/2026 Duration: 09min

    Mkutano wa siku tatu wa Serikali za Dunia mwaka 2026 huko Dubai umesisitiza kuhusu udhibiti wa Akili Mnemba, AI, mageuzi ya kidijitali, uchumi endelevu na thabiti duniani.  Viongozi mbalimbali wametoa wito wa kuwepo ushirikiano thabiti wa kimataifa na mifumo mipya ya utawala inayoweza kutazamia changamoto za siku zijazo lakini pia kushughulikia masuala ya pamoja kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, usalama wa mtandao na ukosefu wa usawa wa kiuchumi. Ni mkutano ulioandaliwa kutoka Februari 3-5, 2026. #WorldGovernmentsSummit

  • Ushindani wa mataifa makubwa na mustakabali wa uchumi wa Dunia

    21/01/2026 Duration: 10min

    Msikilizaji mataifa makubwa kama Marekani, China, Urusi na Ulaya yanaendelea kushindana kiuchumi, kuanzia kwenye biashara, teknolojia, nishati na rasilimali. Lakini je, ushindani wao unaathiri vipi uchumi wa dunia? Leo kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi tunajadili, “Athari za Kiuchumi kwa Dunia Zitokanazo na Ushindani wa Maslahi ya Kiuchumi kati ya Mataifa Makubwa.”

  • Kenya Kuwa Singapore ya Afrika: Ndoto au Uhalisia?

    14/01/2026 Duration: 09min

    Msikilizaji Rais wa Kenya, William Ruto, ameendelea kusisitiza azma ya kuifanya nchi yake kuwa Singapore ya Afrika, suala ambalo limeibua mjadala mkali nchini humo baadhi wakisema ni suala ambalo halitawezekana chini ya utawala wake na wengine wakiona ni jambo linalowezekana. Kwenye makala yetu leo tunajiuliza, je, Kenya inaelekea huko? Ndoto hii inawezekana au ni siasa?

  • Kutoka Ufugaji wa Mifugo hadi Samaki: Mabadiliko ya Kiuchumi Kajiado

    07/01/2026 Duration: 09min

    Msikilizaji jamii ya Wamaasai kwa muda mrefu imekuwa ikitegemea ufugaji wa mifugo kama chanzo kikuu cha riziki na chakula, hata hivyo, mabadiliko ya tabianchi yaliyoambatana na ukame wa mara kwa mara yamilazimisha jamii hii kutafuta mbinu mbadala za kujipatia kipato, mojawapo ni ufugaji wa samaki.

  • Sherehe za mwisho wa mwaka zisikuache bila pesa, fahamu mbinu za kudhibiti matumizi yako.

    24/12/2025 Duration: 10min

    Tunapofika mwisho wa mwaka, jamii huingia katika kipindi cha sikukuu kama krismasi na mwaka mpya, ni wakati wa furaha, sherehe na kukutana na familia, lakini pia ni kipindi ambacho matumizi ya fedha huongezeka, watu wengi hujikuta wakitumia zaidi ya uwezo wao na mipango kusimama, tunajadili namna gani unaweza kuwa na nidhamu ya matumizi ya mwisho wa mwaka iwe kwa muajiriwa, mjasiriamali au mfanyabiashara.

  • Ripoti ya Oxfam-Kenya: Uchumi unakua, lakini Wakenya wengi ni masikini, kwa nini?

    03/12/2025 Duration: 09min

    Msikilizaji juma lililopita shirika la kimataifa la kupambana na umasikini, OXFAM nchini Kenya, ilichapisha ripoti inayoonesha kuongezeka kwa pengo la usawa. Kwa mujibu wa shirika hilo, pengo la walionacho na wasio nacho linaendelea kuongezeka ambapo matajiri 125 wa Kenya kwa sasa wana utajiri wa zaidi ya watu milioni 42 raia wa Kenya. Tunajiuliza, kwa nini ukuaji wa uchumi hauwahusu watu wengi?

  • Mapinduzi ya Elimu Bondo: Jinsi Teknolojia Inavyowawezesha Wasichana Kuandika Kesho Yao

    26/11/2025 Duration: 10min

    Katika maeneo mengi nchini, hasa magharibi mwa Kenya, wasichana wengi wanaojikuta wakisuasua katika mitihani ya sekondari huishia kwenye ndoa za mapema na mimba za utotoni—mazingira yanayozima ndoto zao kabla hata hazijachanua. Lakini safari hii, upepo wa mabadiliko umeanza kuvuma. Serikali za majimbo, kwa ushirikiano na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), zimeanzisha mpango wa mafunzo ya kitaaluma yanaotumia teknolojia ya kisasa, Lengo likiwa ni moja tu, kuwainua wasichana hawa.

  • Mandale: Kinywaji Cha Asili Kinachowainua Wanawake wa Goma

    19/11/2025 Duration: 10min

    Msikilizaji katika uhalisia mgumu wa maisha ya wakazi wa Goma, hususan baada ya mji huo kuangukia mikononi mwa waasi wa AFC/M23, imeibuka hadithi ya kipekee ya uvumilivu na ubunifu wa wanawake. Kati ya changamoto za ukosefu wa ajira na kuyumba kwa uchumi wa familia, wanawake kwenye mji huo wamegeukia ujuzi wa jadi wa kutengenezaji wa kinywaji cha asili kinachoitwa Mandale.

  • Nini hatma ya Afrika baada ya kumalizika kwa mkataba wa kibiashara na Marekani ‘AGOA’

    01/10/2025 Duration: 10min

    Mkataba wa kibiashara kati ya Afrika na Marekani maarufu kama AGOA umefika tamati, ni mkataba uliokuwa unatoa fursa kwa nchi za Afrika kufikia soko la Marekani bila vikwazo vya kiushuru, bara hili likitengeneza faida ya mabilioni ya dola kupitia mkataba huu, hata hivyo kukoma kwake tayari kunashuhudiwa athari yalke kwenye baadhi ya nchi, kuanzia katika viwanda vya nguo nchini Kenya hadi kwa wasafirishaji huko Ghana, maisha ya watu walioajiriwa kupitia mkataba huu yako mashakani.

  • Vijana na ujasiriamali Afrika Mashariki: Nini kifanyike kuwawezesha?

    24/09/2025 Duration: 10min

    Msikilizaji katika nchi zote za Afrika Mashariki, kuna wimbi jipya la matamanio kuhusu hali ya biashara, vijana, wakiongozwa na ubunifu na ustahimilivu! Wakigeuza harakati zao kuwa biashara zinazostawi, kubadili changamoto kuwa fursa na ndoto kuwa ukweli. Tutazungumza na Andrew Lukuwi, yeye ni mjasiriamali kijana akiwa nchini Tanzania, pamoja na Dr Onesmo Kyauke mchambuzi wa masuala ya uchumi na siasa akiwa Tanzania.

  • Mzunguko haramu wa Fedha: Kizuizi kisichoonekana kwa ustawi wa Afrika

    03/09/2025 Duration: 10min

    Kulingana na ripoti ya umoja wa Afrika, bara hilo linapoteza takribani dola za Marekani bilioni 88 kila mwaka kupitia njia zisizo halali kama ukwepaji kodi, utakatishaji fedha, utoroshaji wa mali na mitaji na udanganyifu kwenye biashara. Kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajiuliza, Kwanini hali hii inaendelea licha ya uwepo wa sheria kali? Nani anafaidika? na nini kifanyike kuzuia upotevu huu mkubwa wa rasilimali fedha? Tutakuwa na wataalamu Walter Nguma na Dr Ponsian Ntui.

  • Kuwekeza katika Uchumi wa Bluu: Mkakati wa uhakika au Kamari hatari?

    27/08/2025 Duration: 10min

    Leo hii tunatupia jicho uchumi wa bluu, eneo la kiuchumi linalotajwa kama suluhisho jipya la maendeleo endelevu, kukuza ajira na ubunifu, hata hivyo chini ya uso wa maji, maswali magumu yanajitokeza: Je, tunawekeza kimkakati kwa kuzingatia pia jamii zinazozunguka maeneo haya? Tutazungumza na Dr Ponsian Ntui mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino cha jijini mwanza nchini Tanzania, maarufu kama SAUT.