Synopsis
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .
Episodes
-
Umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na uma
04/03/2024 Duration: 10minShughuli za sekta binafsi na uwekezaji ni vyanzo vikuu ya ukuaji wa uchumi, uzalishaji wa ajira na maendeleo endelevu.Kwa wastani, sekta binafsi inachangia zaidi ya Asilimia 80 ya mapato ya serikali kwa watu wa kipato cha chini na cha kati, kupitia kodi ya kampuni, kodi ya rasilimali na mapato ya kodi kwa wafanyakazi.Sekta hii inazalisha zaidi ya asilimia 90 ya ajira katika nchi zinazoendelea kiuchumi.
-
Ukulima wa matunda Kenya na changamoto zake
04/03/2024 Duration: 10minMakala ya Gurudumu la Uchumi, juma hili inaangazia kilimo cha matunda nchini Kenya, na namna wakulima wa nchi hiyo, wameendelea kukumbatia mbinu mpya za kilimo, uvunaji na usindikaji.
-
Changamoto za uhamiaji na fursa zake kwa uchumi
04/03/2024 Duration: 10minUhamiaji unaweza kuwa nguzo muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa Afrika ikiwa mtu anaweza kutoa mwelekeo bora wa fedha zinazotumwa na wageni kuelekea uwekezaji na ufadhili wa maendeleo katika nchi za Afrika.Diasporas wanachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi zetu ambazo kimsingi ni nchi za asili lakini pia nchi mwenyeji. Wanafanya hivyo kwa kuhamisha pesa, ujuzi, teknolojia, mifano ya utawala, maadili, na mawazo. Serikali ya Senegal inafahamu mabadiliko yanayohitajika tunapojitahidi kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na Mkataba wa Kimataifa wa Uhamiaji Salama, Ulio na Utaratibu na wa Kawaida nchini Senegali.
-
Kuberoshwa kwa huduma ya intaneti Kenya na ilivyochochea ubunifu
04/03/2024 Duration: 10minMakala ya Gurudumu la uchumi juma hili, tunaangazia namna maboreshi ya huduma ya Inteneti nchini Kenya imechochea maendeleo, biashara na ustawi wa watu.
Join Now
- Unlimited access to all content on the platform.
- More than 30 thousand titles, including audiobooks, ebooks, podcasts, series and documentaries.
- Narration of audiobooks by professionals, including actors, announcers and even the authors themselves.