Gurudumu La Uchumi

Manufaa na changamoto za mkataba wa biashara huria barani Afrika, AfCFTA

Informações:

Synopsis

Msikiliza mataifa 54 ya Afrika yametia saini mkataba wa biashara huria barani Afrika, mataifa 48 yakitia saini itifaki kuanza kuutekeleza. Huu ni moja ya mikataba mikubwa ya kibiashara duniani, ukitarajiwa kuwaondoa raia milioni 30 kutoka kwenye umasikini na kuongeza mapato ya bara hil hadi kufikia dola bilioni 450 ifikapo mwaka 2030.Kuangazia kwa kina mkataba huu pamoja na hali ya madeni ya nchi za Afrika, tumezungumza na Ali Mkimo, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania.