Habari Za Un

Informações:

Synopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodes

  • Wiki ya Chanjo Duniani yaanza leo 24 hadi 30 Aprili 

    24/04/2024 Duration: 01min

    Leo ni siku ya kwanza ya siku saba za Wiki ya Chanjo Duniani.(Taarifa ya Anold Kayanda)Wiki ya Chanjo Duniani ambayo huadhimishwa katika kila wiki ya mwisho ya mwezi Aprili, inalenga kuangazia hatua za pamoja zinazohitajika na kuhimiza matumizi ya chanjo kuwalinda watu wa rika zote duniani dhidi ya magonjwa.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO linashirikiana na nchi kote ulimwenguni kuhamasisha ufahamu wa thamani ya chanjo na uchanjaji na kuhakikisha kuwa serikali zinapata mwongozo unaohitajika na usaidizi wa kiufundi ili kutekeleza programu za uchanjaji zenye ubora wa hali ya juu.Lengo kuu la Wiki ya Chanjo Duniani ni kwa watu zaidi  na jamii zao kulindwa dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika.WHO inasema chanjo zimesaidia sana ikitolea mfano namna ulimwengu umeweza kutokomeza ugonjwa wa ndui ambapo mtu wa mwisho kuugua ugonjwa huo ni miaka 47 iliyopita.Mwaka huu Wiki ya Chanjo Duniani inaadhimisha miaka 50 ya EPI ambao ni mpango ambao WHO iliuanzisha mwaka 1974 kwa lengo la kufanya chanjo zi

  • Mtu 1 kati ya 5 katika nchi 59 duniani anahitaji hatua za haraka kuepushwa na baa la njaa: FAO

    24/04/2024 Duration: 02min

    Ripoti mpya ya kimataifa iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO kuhusu mgogoro wa chakula duniani inasema karibu watu milioni 282 walio katika nchi 59 walikabiliwa na viwango vya juu vya njaa mwaka 2023. (TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Asante Leah. Kwa hakika ripoti hiyo ya “Mgogoro wa kimataifa wa chakula” GRFC inasema kiwango cha watu wenye njaa duniani kiliongezeka kwa watu milioni 24 kutoka mwaka 2022 hadi 2023 na ni asilimia 21.5 ya watu waliofanyiwa tahimini  na hicho ni kiwango kikubwa sana ukilinganisha na ilivyokuwa kabla ya janga la COVID-19 limesema shirika la FAO likiongeza kuwa idadi ya walio na njaa duniani inaendelea kuongezeka.Ripoti imetaja sababu kuu tatu ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa janga la njaa duniani ambazo ni mosi migogoro na vita ambapo inasema inaathiri katika nchi 20 zilizo na jumla ya watu milioni 135 wanaokabiliwa na njaa zikiwemo Sudan, Yemen na Palestina katika Ukanda wa Gaza.Pili ni matukio mabaya ya hali ya hewa yaliyochangiwa na mabadiliko ya

  • 24 APRILI 2024

    24/04/2024 Duration: 10min

    Karibu kusikiliza jarida hii leo linaangazia masuala mbalimbali ikiwemo ripotoi ya mgogoro wa chakula duniani, kuanza kwa wiki ya chanjo na utoaji chanjo kwa watoto mashinani. 

  • 23 APRILI 2024

    23/04/2024 Duration: 10min

    Hii leo jaridani utasikia kuhusu ushirikishwaji wa vijana katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Maendeleo UNDP.Pia utasikia muhtasari wa habari kuhusu wasaka hifadhi huko nchini Uingereza kuhamishiwa Rwanda, Makaburi ya halaiki huko Gaza na kuongezeka kwa mlipuko wa ugonjwa wakipindi pindu duniani.Kwa upande wa mashinani hii leo utasikia kuhusu harakati za mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali katika kuhakikisha usalama wa mipaka.

  • Rein Paulsen: Wakati wa kuchukua hatua kuepusha baa la njaa Sudan ni sasa

    22/04/2024 Duration: 03min

    Katika mahojiano na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, afisa mwandamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) anayehusika na masuala ya dharura na mnepo, Rein Paulsen ametahadharisha kuwa hatari ya kutokea baa la njaa nchini Sudan ni halisi na kwa hivyo wakati wa kuchukua hatua ni sasa. Sabrina Moshi anasimulia.

  • DRC: WFP waomba msaada wa $Mil 425 kusaidia wakimbizi wa ndani

    22/04/2024 Duration: 01min

    Wakati Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemorkasia Kongo DRC ikiripoti kuwa na zaidi ya wakimbizi wa ndani 738,000 kwa kipindi cha mwaka huu wa 2024 pekee kutokana na kuongezeka kwa machafuko, Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limeeleza kuwa na uhitaji wa haraka wa dola milioni 425 ili waweze kuwasaidia wakimbizi hao wanaoongezeka kila uchao. Mratibu wa masuala ya dharura wa WFP huko mashariki mwa DRC Bi. Cynthia Jones amesema  hapo awali walipata bahati ya kuanzisha mpango ambapo walikuwa wanaweza ama kuwapatia wakimbizi wa ndani chakula au kuwapatia fedha taslimu na hiyo iliwaruhusu kutoa aina thabiti zaidi ya usaidizi lakini kwa sasa hali ilivyo watalazimika kufanya maamuzi magumu. “Sasa hivi tulikuwa katika hali ambayo tunajitahidi kufikia watu milioni 1.2 na sasa tuna wakimbizi wengine milioni 1.2 wameongezeka. Na kwa hivyo itamaanisha tunapaswa kufanya maamuzi magumu juu ya jinsi tunavyotanguliza nani atakula na nani asile. Tunajaribu kuchukua rasilimali tulizo nazo na kuzit

  • 22 APRILI 2024

    22/04/2024 Duration: 12min

    Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya hali ya joto dunianina madhara yake kwa afya na wafanyakazi, Naomi la ufadhili kwa ajili ya wakimbizi wa ndani DR Congo. Makala tunakupeleka nchini Sudan na mashinani nchini Sudan Kusini, kulikoni? Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa duniani ILO, inasema zaidi ya asilimia 70 ya wafanyakazi wote duniani wanakabiliwa na uwezekano wa hatari za kiafya kutokana na mabadiliko ya tabianchi.Wakati Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemorkasia Kongo DRC ikiripoti kuwa na zaidi ya wakimbizi wa ndani 738,000 kwa kipindi cha mwaka huu wa 2024 pekee kutokana na kuongezeka kwa machafuko, Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limeeleza kuwa na uhitaji wa haraka wa dola milioni 425 ili waweze kuwasaidia wakimbizi hao wanaoongezeka kila uchao.  Katika mahojiano na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, afisa mwandamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) anayehusika na masuala ya dharura na mnepo, Rein Paulsen ametahadharish

  • ILO: Joto la kupindukia linaathiri asilimia 70 yawafanyakazi kote duniani

    22/04/2024 Duration: 02min

    Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa duniani ILO, inasema zaidi ya asilimia 70 ya wafanyakazi wote duniani wanakabiliwa na uwezekano wa hatari za kiafya kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Asante Anold, akizungumza na waandishi wa habari hii leo mjini Geneva Uswis wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo Manal Azzi, afisa wa masuala ya usalama kazini na afya wa shirika la ILO amesema takwimu hizi za kustaajabisha zinasisitiza haja kubwa ya kurekebisha hatua zilizopo za usalama na afya kazini ili kushughulikia ipasavyo vitisho vinayojitokeza kutokana na hatari zinazohusiana na changamoto za hali ya hewa.Ameongeza kuwa “Zaidi ya asilimia 70 ya wafanyakazi wetu wanakabiliwa na joto jingi, angalau joto la kupindukia, katika wakati mmoja wa maisha yao ya kazi. Hiyo ni jumla ya wafanyakazi bilioni 2.4 duniani kote, kati ya wafanyakazi wa kimataifa wa bilioni 3.4.”Ripoti hiyo iliyopewa jina “Kuhakikisha usalama na afya kazini katika mazingira yanayobadilika” inaeleza kwamba mabadiliko ya tabi

  • Lugha ya kichina imepanua fursa za ajira kwa wanafunzi wa SAUT

    20/04/2024 Duration: 05min

    Lugha ni miongoni mwa njia za kimsingi za kujenga utangamano duniani. Umoja wa Mataifa unatambua kuwa lugha ni chombo cha kusongesha tamaduni na miongoni mwa lugha zilizotengewa siku mahsusi kusherehekewa ni kichina ambacho shamrashamra zake ni tarehe20 mwezi Aprili ya kila mwaka.Lugha hii imesambaa duniani ikiwemo Tanzania ambako hii leo Sabrina Moshi wa redio washirika SAUT FM ya mkoani Mwanza kaskazini magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki amefuatilia mafunzo yake kwenye Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino.

  • 19 APRILI 2024

    19/04/2024 Duration: 14min

    Ushirikiano wa kimataifa utasaidia kufanikisha kuhamia katika nishati jadidifu - Francesco La Camera.Vijana wa Afrika lazima tuchangamkie fursa na kujifunza: Joram Nkumbi na Vivian Joseph.Lugha ya kichina imepanua fursa za ajira kwa wanafunzi wa SAUT – Tanzania.Mashinani ni nchini Kenya kusikia jinsi ambavyo mafunzo ya ukulima endelevu na mikopo ya fedha katika mzunguko wa kijamii (Merry-go) inavyowasaidia wakulima kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

  • Jifunze Kiswahili: Tofauti ya maneno “Adhiri na hadhiri.”

    18/04/2024 Duration: 01min

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adhiri; na  hadhiri.”

  • 18 APRILI 2024

    18/04/2024 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina amabyo hivi karibuni tulizungumza na Peter Mmbando kutoka Tanzania akifafanua nini wanafanya ili kuimarisha matumizi endelevu ya teknolojia ya kidijitali. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi na tofauti ya maneno “Adhiri; na  hadhiri."Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameelezea hofu yao juu mwenendo wa mashambulizi dhidi ya shule, vyuo vikuu, waalimu na wanafunzi kwenye Ukanda wa Gaza hali ambayo wamesema ni ishara ya mpango wa uharibifu mkubwa wa mfumo wa elimu wa Palestina.Muungano wa chanjo duniani GAVI na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wamekaribisha taarifa kwamba chanjo mpya ya matone ya kipindupindu Euvichol-S, sasa imepokelewa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na inaweza kupatikana katika nchi mbalimbali duniani. Kupitishwa kwa chanjo hiyo mpya kutasaidia kuongeza usambazaji wake kwa takriban dozi milioni 50 mwaka huu ikilinganishwa na dozi milioni 38 zilizosambazwa mwaka 2023.  Mkutano wa Wiki ya Ue

  • Vijana wakiwezeshwa wanaweza kuvumbua teknolojia ya kusongesha malengo ya maendeleo endelevu

    17/04/2024 Duration: 08min

    Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika jukwaa la vijana la Baraza la kiuchumi na kijamii ECCOSOC ambalo linatoa ukumbi wa kimataifa wa mazungumzo kati ya nchi wanachama na viongozi vijana kutoka kote ulimwenguni kujadili suluhu za changamoto zinazoathiri ustawi wa vijana. Hafla hii pia hutumika kama nafasi ya kipekee kwa vijana kushiriki maono na hatua zao ili kuharakisha utekelezaji wa Ajenda ya 2030 na SDGs ikiwemo masuala ya uvumbuzi na teknolojia. Miongoni mwa wanaohuduria jukwaa hilo kutoka Tanzania ni Vivian Joseph Afisa tabibu na mkuu wa wa kitengo cha afya akiwasilisha vijana katika jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC na Joramu Nkumbi mkurugenzi mtendaji wa jukwaa la Afrika la viongozi vijana kwa upande wa Tanzania. Wameketi na Flora Nducha na kumweleza walichoambulia hadi sasa katika jukwaa hilo litakalokunja jamvi kesho..

  • Mapigano na mizozo DR Congo yanyima wananchi manufaa ya utajiri wa nchi yao - Türk

    17/04/2024 Duration: 02min

    Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk ambaye yuko katika ziara rasmi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amestaajabu ni kwa vipi utajiri wa maliasili uliosheheni kwenye taifa hilo umeleta manufaa kidogo kwa wananchi wako kutokana na ghasia na mapgano. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Video ya Umoja wa Mataifa inaanzia Kinshasa mji mkuu wa DRC ambako Bwana Türk na aafisa mmoja wa Umoja wa Mataifa wanatazama ramani ya taifa hilo lililoko Maziwa Makuu na kisha anasema ni moja ya nchi tajiri zaidi duniani, lakini tunaona ni kwa vipi utajiri huu kwa bahati mbayá hauko kunufaisha wananchi kwa sababu ya mapigano.Na kisha anaelezea mipango ya ziara yake ya kutathmini hali ya haki za binadamu akisemakwanza ni kukutana na watu waliofurushwa makwao kutokana na ghasia na vile vile kuonana na mamlaka husika na mashirika ya kiraia.Baada ya hapo safari inaanza akiambatana na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Bintou Keita, mwelekeo ni Mashariki mwa nchi

  • 17 APRILI 2024

    17/04/2024 Duration: 13min

    Hii leo jaridani tunaangazia ghasia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na jitihada za Umoja wa Mataifa za kukwamua hali ya Kibinadamu nchini Ethiopia. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunaelekea nchini Madagascar, kulikoni?Kaminshna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk ambaye yuko katika ziara rasmi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amestaajabu ni kwa vipi utajiri wa maliasili uliosheheni kwenye taifa hilo umeleta manufaa kidogo kwa wananchi wako kutokana na ghasia na mapgano.Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Kutoa ahadi kwa ajili ya ufadhili wa kukwamua hali ya Kibinadamu nchini Ethiopia uliokamilika jana mjini Geneva, Uswisi umetangaza kwamba wafadhili 20 wametangaza msaada wa kifedha wa Dola za Marekani milioni 610 angalau kuhakikisha misaada kwa miezi michache ijayo.  Makala inaturejesha hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kunakofanyika jukwaa la vijana la Baraza la kiuchumi na kijamii ECCOSOC ambalo linatoa ukumbi wa kimataifa wa mazungumzo kati ya nch

  • Mkutano wa ufadhili wapata msaada wa fedha wa dola milioni 610 kwa ajili ya Ethiopia

    17/04/2024 Duration: 01min

    Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Kutoa ahadi kwa ajili ya ufadhili wa kukwamua hali ya Kibinadamu nchini Ethiopia uliokamilika jana  mjini Geneva, Uswisi umetangaza kwamba wafadhili 20 wametangaza msaada wa kifedha wa Dola za Marekani milioni 610 angalau kuhakikisha misaada kwa miezi michache ijayo.Mkutano huo uliolenga kukusanya dola bilioni 1 za kimarekani kwa ajili ya miezi mitano ijayo, ulikuwa umeandaliwa kwa pamoja kati ya Umoja wa Mataifa, Serikali ya Ethiopia na Uingereza, na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa masuala ya kibinadamu.  Mara tu baada ya mkutano huo Naibu Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura OCHA, Joyce Msuya, aliwashukuru wafadhili hao na kusema kuwa huo ni mwanzo tu na matumaini ni kuendelea na kuongeza msaada kwa mwaka mzima.Dharura ya kibinadamu nchini Ethiopia imekuwa ikiongezeka kupitia mizunguko ya ukame na mafuriko, na migogoro. Ukosefu wa uhakika wa chakula na utapiamlo unatarajiwa kufikia kiwango cha juu kwa watu milioni 10.8 wakati

  • 16 APRILI 2024

    16/04/2024 Duration: 12min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Tanzania, Abeida Rashid Abdallah anafafanua kwa nini Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Zanzibar ni chanda na pete.  Pia tunakuletea muhtasari ya habari na mashinani kama zifuatazo.Leo mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kuonya juu ya vita inayoendelea kukatili maisha ya watu Gaza, na kusambaratisha miundombinu yakitaja kuwa wanawake karibu 10,000 wamepoteza Maisha tangu vita kuanza miezi sita iliyopita huku mtoto mmoja anajeruhiwa au kuuawa kila dakika 10.Jukwaa la vijana la Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC leo limeng’oa nanga hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Matrekani likiwaleta maelfu ya vijana kutoka kila kona ya Dunia. Joramu Nkumbi ni miongoni mwa washiriki wa jukwaa hilo kutoka Tanzania na anafafanua wanachokijadili mwaka huu.  Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM kwa shirikiana na mashirika mengine 48 y

  • Ni dhana potofu kudai Wamaasai wanaua Simba ili kupata mke - Alois Porokwa

    15/04/2024 Duration: 03min

    Katika harakati za kupambana na mabadiliko ya tabianchi, kuna wakati jamii ambazo bado zinaishi kiasili zimekuwa zikilaumiwa kwamba zinachangia kuharibu mazingira kutokana na wao kuishi katika mazingira fulani; mathalani misitu na mbuga jambo ambalo linakanushwa na jamii hizo wakidai kwamba kimsingi wao ndio watunzaji wazuri wa mazingira kwani wanayategemea moja kwa moja kwa mustakabali wa maisha yao ya kila siku na siku zijazo. Hivi karibuni wakati wa Mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6 uliofanyika jijini Nairobi, Kenya, Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Kenya, Stella Vuzo alimhoji Alois Porokwa, Mkurugenzi wa shirika la NALEPPO kutoka jamii ya Wamaasai aliyesafiri kutoka Kijiji cha Emboreet, Wilaya ya Simajiro, Mkoa wa Manyara, Tanzania. Ni katika mazungumzo hayo ndipo Stella Vuzo akakumbuka kumuuliza Alois Porokwa swali hili ambalo ni dhana inayohusisha jamii ya Wamaasai kuua wanyama.

page 3 from 5