Habari Za Un

UNHCR: Chonde chonde jumuiya ya Kimataifa tuishike mkono Uganda kwa faida ya waomba hifadhi na wakimbizi

Informações:

Synopsis

Mwaka 2024 ukielekea ukingoni, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR  nchini Uganda limetoa rai kwa jumuiya ya kimataifa kutolisahau taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo ni maskani ya idadi kubwa zaidi ya waomba hifadhi na wakimbizi barani Afrika. Rai hiyo iliyotolewa mwishoni mwa wiki inataka ufadhili wa fedha uongezwe ili liweze kuendelea kukirimu watu hao ambao wengi wanakimbia machafuko. Huyo ni Moulid Hujale afisa wa UNHCR nchini Uganda akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kushikamana na Uganda akiwa  kwenye makazi makubwa ya wakimbizi ya Kiryandongo Magharibi mwa nchi hiyo. Anasema kuna mambo matatu muhimu ambayo dunia inapaswa kufahamu kuhusu Uganda na wakimbizi.“Mosi Uganda inahifadhi idadi kubwa zaidi ya wakimbizi na waomba hifadhi Afrika ikiwa na zaidi ya watu milioni 1.7 wengi wao wakitoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Sudan Kusini.”Zaidi ya hapo ukarimu wa Uganda anasema hauna kipimo“Pili, Uganda ina sera ya kufugua mlango kwa wakimbizi na pia kwa miong