Sbs Swahili - Sbs Swahili

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 107:51:01
  • More information

Informações:

Synopsis

Listen to interviews, features and community stories from the SBS Radio Swahili program, including news from Australia and around the world. - Sikiza mahojiano, makala na hadithi za jumuiya kutoka Idhaa ya Kiswahili ya SBS Radio, ikijumuisha taarifa za habari kutoka Australia na ulimwenguni.

Episodes

  • Taarifa ya Habari 3 Januari 2025

    03/01/2025 Duration: 18min

    Kufanya mfumo wa afya upatikane kwa bei nafuu itakuwa sehemu kubwa ya kampeni ya uchaguzi mkuu ya chama cha Labor, waziri wa afya washirikisho aki ahidi kuimarisha Medicare miongoni mwa hatua zingine kabla ya mwanzo wa kampeni.

  • Je uchaguzi wa uongozi uta sababisha mpasuko ndani ya CHADEMA

    03/01/2025 Duration: 08min

    Wanachama wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, wanasalia na takriban wiki mbili kuingia debeni kumchagua kiongozi mpya.

  • Taarifa ya Habari 31 Disemba 2024

    31/12/2024 Duration: 20min

    Kikundi cha magari cha N-R-M-A kina omba tume ya ushindani na watumiaji ya Australia, ifanye uchunguzi wa haraka kwa madhara mabaya ya mizunguko ya bei bei ya petroli katika miji mikubwa ya Australia.

  • Levi "Wazazi wasi harakishe kuwatuma watoto ng'ambo kabla hawaja komaa"

    31/12/2024 Duration: 20min

    Wazazi wengi huwa na ndoto za kuwatuma watoto wao ng'ambo kufanya elimu ya juu.

  • Taarifa ya habari 27 Disemba 2024

    27/12/2024 Duration: 16min

    Mabadiliko mazuri ya hali ya hewa yame saidia juhudi za wazima moto wanao kabiliana na moto ambao haukuwa ukidhibitika katika maeneo ya Grampians jimboni Victoria, baada ya hali mbaya zaidi ya hali ya hewa kwa moto wa vichaka tangu tukio la Black Summer la 2019.

  • Jeshi la polisi la Kenya lakanusha kuhusika na utekaji wa wakosoaji wa serikali

    27/12/2024 Duration: 08min

    Jeshi la polisi Kenya limekanusha kuhusika na visa vya karibuni vya utekaji unaowalenga wakosoaji wa serikali. Watu 74 walitekwa tangu maandamano ya kuipinga serikali, huku 26 wakiwa bado hawajulikani waliko.

  • Understanding Indigenous knowledge of weather and seasons - Kuelewa maarifa ya hali ya hewa na misimu yawatu wa asili

    27/12/2024 Duration: 10min

    You’re probably familiar with the four seasons—Summer, Autumn, Winter, and Spring—but did you know that First Nations people have long recognised many more? Depending on the location, some Indigenous groups observe up to six distinct seasons each year. - Pengine unafahamu misimu minne- Majira ya joto, vuli, majira ya baridi na masika ila, unafahamu kuwa watu wa Mataifa ya Kwanza wame tambua misimu mingine mingi kwa muda mrefu? kutegemea na sehemu, baadhi ya vikundi vya watu wa asili, hushuhudia takriban misimu sita tofauti kila mwaka.

  • Taarifa ya Habari 26 Disemba 2024

    27/12/2024 Duration: 06min

    Mamlaka wa Urusi na Australia wachunguza ripoti kuwa, raia wa Australia amekamatwa akipigania Ukraine.

  • Taarifa ya Habari 24 Disemba 2024

    24/12/2024 Duration: 19min

    Waziri Mkuu Anthony Albanese ametupilia mbali tathmini ya upinzani kuwa amefeli kwa swala la uhamiaji, wakati ripoti za mihadarati kama heroin, methamphetamine na fentanyl kuingia katika vizuizi vya uhamiaji vya Australia.

  • Wangeci "nilikuwa mkali sana katika mawasiliano yetu ya kwanza"

    24/12/2024 Duration: 17min

    Je, unakumbuka ulipo mwona mpenzi wako mara ya kwanza? alikupokea ulivyo tarajia, au ilibidi uboreshe mstari yako kabla ujaribu tena?

  • Kuelewa maarifa ya wa Australia wa Kwanza kuhusu hali ya hewa na misimu

    22/12/2024 Duration: 11min

    Pengine unafahamu misimu minne- Majira ya joto, vuli, majira ya baridi na masika ila, unafahamu kuwa watu wa Mataifa ya Kwanza wame tambua misimu mingine mingi kwa muda mrefu?

  • Kauli ya mwanae Museveni yazua kero kwa majirani Sudan na DRC

    20/12/2024 Duration: 06min

    Serikali ya Sudan inaitaka Uganda iombe rasmi msamaha, kutokana na kile imekitaja kuwa ujumbe wa kuchukiza na hatari ulioandikwa na mkuu wa jeshi la Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba, aliyetishia kuivamia Khartoum kijeshi.

  • Bw Chumba "tukishikana mikono itatupa urahisi kufanya vitu vikubwa pamoja"

    20/12/2024 Duration: 08min

    Viongozi wa Jumuiya yawa Kalenjin wanao ishi New South Wales wanajiandaa kuwasilisha vyeti vya usajili wa Jumuiya kwa wanachama wao jioni ya Ijumaa 20 Disemba 2024.

  • Taarifa ya Habari 20 Disemba 2024

    20/12/2024 Duration: 18min

    Eneo la kusini mashariki Queensland, lina jiandaa kukaribisha afueni ya hali ya hewa baada ya dhoruba kusababisha barabara kufungwa, umeme kupotea na mafuriko.

  • Mchungaji Mgogo "tunza ujana wako kwa ajili ya future yako"

    20/12/2024 Duration: 14min

    Mchungaji Daniel Mgogo ni maarufu sana katika mitandao yakijamii, kwa jinsi anavyo huburi.

  • Taarifa ya Habari 17 Disemba 2024

    17/12/2024 Duration: 20min

    Mawaziri wa kigeni na ulinzi wa Uingereza na Australia wamefanya mkutano wao wa kila mwaka ((AUKMIN)) mjini London ambako amekubali kuimarisha zaidi ushirikiano kwa ulinzi, biashara na sera yakigeni.

  • Mahakama yazima ndoto ya Edgar Lungu

    13/12/2024 Duration: 07min

    Mahakama ya katiba ya Zambia imesikiza ombi la Rais mstaafu wa Zambia, Edgar Chagwa Lungu lakupewa ruhusa yakuwania urais wa taifa hilo.

  • Taarifa ya Habari 13 Disemba 2024

    13/12/2024 Duration: 22min

    Serikali ya Albanese imetangaza mfumo mpya waku lazimisha mitandao yakidigitali yakufidia vyombo vya utangazaji vya Australia kwa matumizi ya habari zao.

  • Kuelewa uhusiano wa kina wa Mataifa ya Kwanza na ardhi

    10/12/2024 Duration: 08min

    Ardhi ina umuhimu mkubwa wa kiroho kwa wa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait, iliyo unganishwa kwa ustadi na utambulisho wao, kuwa sehemu na hali yao ya maisha.

  • Taarifa ya Habari 10 Disemba 2024

    10/12/2024 Duration: 16min

    Waziri wa Huduma za Serikali Bill Shorten ametangaza kuwa shirika la Services Australia, lime tekeleza karibu nusu ya mapendekezo yote kutoka Tume yakifalme kwa mfumo usio halali wa Robodebt.

page 1 from 26