Synopsis
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
Episodes
-
Dunia yaukaribisha mwaka mpya wa 2025 huku viongozi wakiomba amani
01/01/2025 Duration: 10minMataifa mbalimbali duniani wakiwemo raia wa ukanda wa Afrika Mashariki, wamesherehekea mwaka mpya wa 2025 kwa kila aina ya mbwembwe na shamrashamra, kukiwa na hisia mseto za matumaini tofauti na mwaka uliopita.Tulimuuliza mskilizaji atueleze aliukaribisha mwaka mpya vipi na akiwa wapi,vile vile angependa kuona kipi kinabadilika kwenye nchi yake.
-
Matumizi ya mitandao ya kijamii nchini Kenya yaibua hisia mbalimbali
31/12/2024 Duration: 10minNchini Kenya mjadala mkali kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii unaendelea, ambapo baadhi wamekuwa wakiitumia kuikosoa Serikali na rais William Ruto, kwa kiwango ambacho wengine wanasema wakosoaji wamevuka mipaka huku baadhi wakisema watu wako huru kukosoa wanavyotaka.Tulimuuliwa mskilizaji je anaamini iwapo vijana wamevuka mipaka au la.
-
Umoja wa mataifa,waidhinisha kikosi kipya cha kulinda amani nchini Somalia
30/12/2024 Duration: 10minBaraza la usalama la umoja wa Mataifa, mwishoni mwa juma limepitisha azimio kuunga mkono uundwaji wa kikosi kipya cha bara Afrika cha kulinda amani nchini Somalia, kikosi hiki kikichukua nafasi ya kile cha ATMIS na kitakuwa na jukumu la kuwakabili wanamgambo wa Al-Shabaab.Tumemuliza msikilizaji iwapo anaamini kikosi hiki kipya kitafanikiwa kuleta amani nchini Somalia
-
Morocco yapendekeza wanawake kurithi mali na muda wa kuolewa kuongezwa
26/12/2024 Duration: 10minSerikali ya Morocco imependekeza marekebisho ya sheria kuwaruhusu wanawake kurithi mali, umri wa kuolewa kuongezwa kutoka 17 hadi 18 na kuwekwa kwa masharti kwa wanaume wanaotaka kuoa mwanamke zaidi ya mmoja.Tunamuuliza msikilizaji maoni yake kuhusu mapendekezo hayo na hali iko vipi nchini mwake kuhusu wanawake urithi mali
-
Krisimasi: Mamia ya wasafiri Kenya wakwama barabarani wakielekea sikukuu
24/12/2024 Duration: 09minMamia ya wasafiri wanaoelekea maeneo mbalimbali kwa sherehe za Krismasi wamekwama barabarani nchini Kenya kutokana na msongamano mkubwa wa magari na wengine kukosa magari ya usafiri wa umma.Tunamuuliza msikilizaji nini kinasababisha kuongezeka kwa safari msimu wa sikukuu na nchini mwao hali ikoje.
-
Habari Rafiki: Somalia kuongoza Kikosi cha Kudumu cha Afrika Mashariki
23/12/2024 Duration: 09minKwa mara ya kwanza katika historia yake, Somalia itaongoza Kikosi cha Kudumu cha Afrika Mashariki (EASF) ambacho kimetwikwa jukumu la kuimarisha amani na usalama katika eneo hilo baada ya kuchukua uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Ulinzi wa jumuiya hiyo kutoka nchi ya Rwanda katika hafla iliyofanyika jijini Kigali hapo jana.Tunamuuliza msikilizaji maoni yake ni yepi kuhusiana na hatua hii.
-
Maoni ya mskilizaji kuhusu taarifa zetu juma hili
20/12/2024 Duration: 09minRFI Kiswahili kila siku ya Ijumaa inakupa nafasi ewe msikilizaji wetu kuchangia mada yeyote uliyoiskia kwenye habari zetu au kile kinachoendelea hapo ulipo. Haya ndio maoni ya waskilizaji wetu juma hili.
-
Mahakama nchini Kenya yaamuru msichana wa miaka 16 anayekiri kushiriki ngono si unyanyasaji
18/12/2024 Duration: 09minWasikilizaji watoa maoni kuhusu hatua ya Mahakama moja nchini Kenya, kuamuru kwamba msichana wa umri wa miaka 16 anayekiri kushiriki ngono na mwanaume si thibitisho la unyanyasaji wa kigono, uamuzi ambao umeibua hisia kali nchini Kenya.
-
Rais wa Uturuki Recep Erdogan kuzuru Ethiopia na Somalia Mwakani
18/12/2024 Duration: 10minHujambo karibu katika makala ya Habari Rafiki ambapo wasikilizaji walizungumzia tangazo la Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Edorgan,kuwa atazuru Ethiopia na Somalia mwakani, baada ya kupatanisha mataifa hayo mawili kufuatia mzozo wa bandari ya Somaliland.
-
Maoni ya wasikilizaji kuhusu habari zilizogonga vichwa vya habari wiki hii
13/12/2024 Duration: 10minHapa wasikilizaji wamezungumzia mkutano kati ya viongozi wa Rwanda na DRC kule Angola wikendi hii, pia vijana kujituma ili kufanya kazi kujikimu kimaisha
-
Tanzania, Uganda na DRC zafuzu kucheza AFCON
22/11/2024 Duration: 10minHujambo na karibu kwenye makala ya habari rafiki, leo tunajadili kufuzu kwa mataifa ya Tanzania Uganda na DRCongo , kucheza kwenye mchuano ya kuwania AFCON, mataifa haya yakiwakilisha Afrika Mashariki nchini Morroco mwaka ujao. Je unazungumziaje kufuzu kwa mataifa haya?Haya hapa baadhi ya maoni.
-
Kenya : Askofu wa kanisa katoliki walaani serikali
19/11/2024 Duration: 09minKatika makala tunajadili hatua ya viongozi wa dini nchini Kenya, kutuhumu serikali kwa kile wamedai imekuwa ikitoa ahadi za uongo kwa raia. Je unazungumziaje kauli hii ya viongozi wa dini nchini Kenya? Haya hapa maoni yako.
-
Sudan : IGAD yapendekeza vikosi kutuma kulinda raia
18/11/2024 Duration: 09minKwenye makala hayai tunajadili hatua ya Jumuiya ya IGAD kuripotiwa kupendekeza kutumwa kwa wanajeshi wa kulinda amani toka nchi za Afrika ambazo hazijajihusisha kwenye mzozo unaoendelea ili kusimamia mkataba wa usitishaji mapigano kati ya jeshi na wapiganaji wa RSF nchini #sudan. Unamtazamo gani kwa pendekezo hili? Haya hapa baadhi ya maoni yako.
-
Maoni ya wasikilizaji kuhusu matukio na habari juma lote ikiwemo COP29
15/11/2024 Duration: 10minMadu huru zilizoangaziwa na wasikilizaji wetu wiki hii
-
Australia imeridhia sheria kuwazuia watoto kutotumia mitandao ya kijamii
14/11/2024 Duration: 10minBunge la Australia limesema mitandao ya kijamii ina madhara makubwa kwa watoto
-
Australia yapitisha sheria ya kuwazuia watoto kutumia mitandao ya kijamii
14/11/2024 Duration: 10minBunge la Australia limesema mitandao ya kijamii ina madhara makubwa kwa watoto
-
Baraza la usalama limejadili mapendekezo ya Uingereza kuhusu mzozo wa Sudan
14/11/2024 Duration: 09minMapendekezo ya taifa la Uingereza yanataka vita kusitishwa nchini Sudan na kuruhusiwa misaada ya kibinadamu kuwafikia waathiriwa.
-
Changamoto zinazoandama mipango ya bima ya afya katika mataifa ya Afrika
12/11/2024 Duration: 10minNchini #kenya ,wagonjwa wengi wanaendelea kutaabika kupata huduma za afya kufuatia changamoto zinazotokana na utekelezwaji wa mpango mpya wa afya ,SHIF Hali hii ndiyo pia inayokumba nchi nyingi za Afrika zinazojaribu kutekeleza mipango ya afya inayosimamiwa na serikali.
-
Viwango vya umaskini nchini Uganda vimeongezeka mno ,yasema ripoti mpya
11/11/2024 Duration: 08minUmaskini umeendelea kukithiri katika baadhi ya maeneo nchini Uganda Ripoti ya shirika moja lisilo la kiserikali nchini #Uganda, inayoonesha kuwa karibu asilimia 68 ya raia nchini humo wanapata ugumu kujikimu kimaisha kutokana umasikini.