Jua Haki Zako

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 3:57:08
  • More information

Informações:

Synopsis

Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.

Episodes

  • Juhudi zilizopo kuondoa hukumu ya kifo kwenye nchi barani Afrika

    21/01/2025 Duration: 10min

    Katika nchi nyingi barani Afrika, adhabu ya kifo inasalia kuwa suala tata, ikiwa imejikita katika mifumo ya kisheria na kijamii. Licha ya mjadala kuhusu ufanisi na maadili yake kuendelea, wanaharakati wa haki za binadamu wanajitahidi kuhakikisha kufutwa kwa adhabu hiyo, wakisisitiza haki ya msingi ya kuishi. Ulaya tayari imeondoa adhabu ya kifo, ikitoa mfano wa mfumo wa haki unaolenga marekebisho badala ya adhabu kali.Kwenye makala haya tumeangazia juhudi hizo kuondoa adhabu hiyo .

  • Kenya: Uhuru wa kutumia mitandao ya kijamii na mipaka yake

    09/01/2025 Duration: 10min

    Siku ya Jumatatu asubuhi Vijana wanne kati ya 6 waliotekwa nyara katika wiki za hivi majuzi waliachiliwa huru, saa chache kabla ya maandamano yaliyopangwa kufanyika kupinga kutoweka kwao.  Billy Munyiri Mwangi na Peter Muteti waliungana na familia zao huko Embu na Nairobi, mtawalia, baada ya kuzuiliwa kwa zaidi ya wiki mbili ilhali Rony Kiplangat alipatikana katika kaunti ya Machakos naye Benard Kavuli akapatikana katika maeneo ya Kitale magaribi mwa nchi. Katika makala Jua haki zako, tunaangazia huru wa kutumia mitandao ya kijamii na katika kutumia mitaoa hiyo kuna mipaka yake. Je nchini Kenya hatua zipi zinafaa kuchukuliwa ikiwa mshukiwa atapatikana na hatia ya kukiuka huru ywa mitandao ya kijamii.

  • Dunia:Haki za wanawake na Ukomeshaji wa visa vya mauaji

    30/12/2024 Duration: 09min

    Makala jua haki zako leo yataangazia haki za kina dada,changamoto wanazopitia na nini wanaharakati wanafanya ili kuhakikisha visa vya dhulma vinaripotiwa kwa wakati na haki inatendeka.Kumbuka killa mwaka, kuanzia tarehe 25 Novemba hadi 10 Disemba, dunia inaungana kwa pamoja kutambua changamoto kubwa zinazowakumba wanawake na wasichana, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia, ukatili wa kifamilia, na vitendo vingine vyote vya ubaguzi na dhuluma.

  • Kenya : Akili dada na Juhudi zake za kuinua maisha ya mtoto wa kike

    18/12/2024 Duration: 10min

    Joy Zawadi, mkurugezi mkuu wa shirika la Akili Dada, linalopigania haki za mtoto wa kike alikiti chini na Benson Wakoli, kujadili juhudi wanazofanya kuinua mtoto wa kike nchini Kenya. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.

  • Kenya : Akila Dada mstari wa mbele kutetea haki za mtoto wa kike

    17/12/2024 Duration: 10min

    Haya ni awamu ya pili ya makala haya, ambapo Joy Zawadi afisa Mtendaji kutoka shirika la Akili Dada, anaendelea kujadili namna gani haki za mtoto wa kike zinaweza kuheshimiwa. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.

  • DRC : Mchango wa AU kumaliza mizozo Africa

    16/12/2024 Duration: 10min

    Moses Balagisi, afisi kutoka shirika la umoja wa Africa linaloshirikiana na masharika ya kiraia, kuhakikisha uongozi wa juu wa AU unaskiza kilio cha raia wa chini, analeza namna gani wanahakikisha hilo linafanyika. Kufahamu mengi zaidi, skiza makala haya.

  • Kenya :Madaktari watishia kugoma tena tarehe 22 Disemba

    09/12/2024 Duration: 10min

    Wahudumu wa afya  nchini Kenya  wanaitaka serikali kuwatuma kazini wanafunzi na wahudumu wa afya mara moja na kufuta malimbikizo ya mishahara ya madaktari kulingana na Makubaliano ya Pamoja ya 2017. Wahudumu wa afya ambao wamehudumu kwa miaka minne chini ya kandarasi katika taasisi za afya ya umma wanadai ajira ya kudumu ambayo walikuwa wamehakikishiwa na serikali ya Kenya kufuatia miaka mitatu ya huduma.

  • DRC : Haki ya mtoto kupata elimu na vizingiti vinavyochangia

    12/11/2024 Duration: 10min

    Katika makala haya tunajadili haki za mtoto kupata elimu nchini DRC, hapa mkuu wa chuo cha walumu cha ISP, Butua Balingane anafafanua vizingiti vya mtoto kupata elumu nchini DRC. Kufahamu mengi skiza makala haya.

  • DRC : Haki ya wanawake kupata elimu

    05/11/2024 Duration: 10min

    Nchini DRC, kumeripotiwa upungufu wa watoto wa kike katika kupata elimu, hili likidaiwa kuchangiwa na tamaduni zilizopitwa na wakati. Katika makala haya basi Butua Balingane, mkurugezi wa chuo kikuu cha walimu cha ISP, Goma ambaye anasimulia masaibu anayopitia mtoto wa kike nchini DRC kupata elimu. Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.

  • Kenya : Wanawake 97 wauawa kwa kipindi cha miezi tatu

    05/11/2024 Duration: 09min

    Nchini Kenya, idara ya polisi imekiri kwamba wanawake 97 wameuawa kwa kipindi cha miezi 3, baadhi miili yao ikipatikana imenyofolewa. Ni visa ambayo vimesababisa viongozi wa ngazi ya juu akiwemo rais William Ruto, ambaye ametoa agizo wa asasi za uchunguzi nchini humo kuwasaka na kuwachukulia hatua wale wote ambao wamehusika katika visa hivyo. Kwenya makala haya tunazama kujadili kile kinachoendelea nchini Kenya, ambapo mtaalamu wa maswala ya jamii bi Carolina Situma anaeleza nini kimechangia mauwaji haya.

  • Kenya : Visa vya raia kutekwa yaongezeka

    25/10/2024 Duration: 09min

    Nchini Kenya, visa vya raia kutekwa na kisha baadaye kuachiliwa au kupatikana wameuawa vinazidi kuongezeka, visa kadhaa vikiendelea kugonga vichwa vya habari. Katika Makala haya George Ajowi angaazia visa hivi na jinsi mkuu wa polisi nchini Kenya alikosa kufika mahakamani kueleza walipokuwa baadhi ya wakenya waliotekwa.

  • Hatua zilizopigwa katika kumuinua mtoto wa kike

    24/10/2024 Duration: 10min

    Katika muendelezo wa makala kuhusu siku ya mtoto wa kike duniani,  tunaangazia vyanzo vya visa vya unyanyasaji wa watoto wa kike na hatua zilizopigwa na mashirika mbalimbali katika kuifanya sauti ya mtoto wa kike kusikika.

  • Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani

    18/10/2024 Duration: 09min

    Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 11 Oktoba, ni fursa ya kuangazia changamoto zinazokabili watoto wa kike duniani na kukuza usawa wa kijinsia. Katika mwaka 2024, mada ilikuwa "Kutoa sauti kwa watoto wa kike: Fursa na Changamoto katika Utu wa Kike."Makala haya yataangazia kwa kina haki za mtoto wa kike na hatua zilizopigwa katika kusababisha mtoto wa kike kuskizwa na hata hatua zilizochukuliwa ili kuboresha elimu, afya, na usalama wa watoto wa kike, pamoja na jinsi jamii zinaweza kushiriki katika kuwasaidia kufikia ndoto zao.Aidha, itajadili umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wazazi katika kufanikisha malengo haya.

  • MAMILLIONI YA WATU HASA WATOTO BARANI AFRIKA HAWAJAPATA HAKI ZA CHAKULA

    16/10/2024 Duration: 09min

    Chakula ni muhimu kwa maisha, kuishi, heshima, ustawi, na maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa  watu binafsi, jamii, na mataifa. Sheria za kimataifa zinatambua haki ya kila mtu kupata chakula cha kutosha na haki ya kuwa huru kutokana na njaa. Haki hii ni ya msingi kwa utekelezaji wa haki zote za binadamu.  Nchini  Kenya, ni haki ya kikatiba, iliyoko  katika Kifungu cha 43(1)(C) kinachosema: "Kila mtu ana haki ya kuwa huru kutokana na njaa na kuwa na chakula  bora na cha kutosha .Lakini je, sheria hii inatambuliwa ? Je, watu wanaelewa haki yao ya chakula? Na hali ya usalama wa chakula nchini Kenya iko vipi leo?Katika kipindi cha leo ,cha jua haki zako , tunaangazia iwapo watu wanapata haki zao za kupata  chakula na jinsi changamoto za kiuchumi na kimazingira zinavyoathiri upatikanaji wa chakula nchini Kenya

  • DRC : Wanawake wabakwa katika gereza la Makala nchini

    19/09/2024 Duration: 09min

    Katika makala haya tunaangazia ripoti ya umoja wa mataifa kusema kwamba zaidi ya wanawake wafungwa ya 260 walibakwa katika jela ya Makala nchini DRC, mapema mwezi huu wakati wa jaribio la wafungwa kutoroka jela. Ripoti hiyo imebaini kwamba kati ya wafungwa 348 katika gereza hilo la Makala, wafungwa 268, walitendewa vitendo vya unyanyasaji wa kingono ikiwemo ubakaji,  wanawake 17 kati ya waliobakwa wakiwa chini ya umri wa miaka 19.Ripoti hiyo aidha imeongeza kuwa wanawake hao walilazimika kutafuta mbinu za kuzuia magonjwa baada ya kutendewa vitendo hivyo vya kikatili.Awali serikali ya DRC ilikuwa imekiri kubakwa kwa wanawake hao ila haikotoa idadi ya wanawake waliobakwa.Kadhalika ripoti hiyo pia imesema wafungwa 129 waliojaribu kutoroka jela waliuawa kwa kupingwa risasi, katika gereza hilo la Makala ambao linastahili kutoa huduma kwa wafungwa 1500, ila lina zaidi ya wafungwa alfu 15.Rais Felix Tshisekedi aliagiza kufanyika kwa uchuguzi kuhusiana na jaribio hilo la wafungwa kutoka, na mikakati ya kupunguza idad

  • Kenya : Watoto wateketea shuleni, je jukumu la nani kumlinda mtoto akiwa shuleni

    16/09/2024 Duration: 09min

    Nchini Kenya zaidi serikali inaendesha uchunguzi wa chembechembe za DNA, za wanafunzi 21 wa shule ya msingi ya Endatasha baada yao kuteketea kiasi ya kutotambulika, kabla ya miili yao kutolewa kwa familia. Miili limewaacha wazazi kwenye njia panda wasijue la kufanya, wakati huu maswali yakiendelea kuulizwa je nani wakulaumiwa baada ya mkasa huo wa moto shuleni. Kufahamu mengi skiza makala haya.

  • Kenya: Vikundi vya kina mama vyajitokeza kupinga ukeketaji

    27/08/2024 Duration: 10min

    Katika makala haya tunajikiti kuangazia uketetetaji ambapo wasichana  wamekuwa ukiendelea kukeketewa nchini Kenya licha ya serikali kanzisha kampeni ya kuhamasisha umma kuhusu athari zinazotokana na ukeketaji huo. Jamii za Kenya, kupitia kwa kina mama na wasichana waliopitia ukeketaji  kwa ushirikiano na mashirika ya kijamii wameanzisha vikundi vya kutetea haki za wasichana ili kuwalinda kutokana na ukeketaji huo. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.

  • Kenya : Jamii za mipakani zataka serikali kuwapa vitambulisho

    24/08/2024 Duration: 09min

    Jamii zinazoishi mikapani nchini Kenya kwa muda zimekuwa  zikikosa huduma muhimu ya kupata vitambulisho kutoka na sababu ambazo wenyewe wanasema serikali inawabagua. Katika makala haya tunajikiti kuangazia masaibu ya jamii za mipakani nchini kenya kupata vitambulisho. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.

  • Kenya : Mawikili watoa mafunzo ya sheria kwa vijana

    17/08/2024 Duration: 09min

    Mawakili mjini Mombasa pwani ya Kenya wamenza kutoa mafunzo ya sheria kwa vijana waliokuwa wakiandamana kushinikiza mabadiliko. Mawakili hao ambao ni wanachama wa chama cha mawakili nchini LSK, wamesema hatua hiyo imechochewa na maandamano yaliokuwa  ya vijana maarufu kama Gen-Z leo lengo lao  kuu likiwa kuwawajibisha viongozi serikalini. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya

  • Tanzania : Human Right Watch lasema Tanzania inawahangaisha raia wa Ngorongoro

    06/08/2024 Duration: 10min

    Katika makala haya saba yetu inalenga taifa la Tanzania eneo la Ngorongoro ambapo serikali imekuwa ikiwahamisha wenyeji eneo hilo, ili kuihifadhi eneo hilo  kutokana na historia yake. Tuangazia repoti ya shirika la kimataifa la kutete haki za biandamu la Human Watch ambayo imetuhumu serikali ya Tanzania kwa kuwafurusha kwa nguvu mamia ya raia wa kimasaai kutoka eneo la Ngorongoro, maafisa wa wanyama pori wakidaiwa kuwahangaisha kwa kuwapiga wenyeji ili kuwafurusha kutoka katika ardhi za mababu zao.Karibu kwenye makala haya utaskia kutoka kwa wadau mbalimbali huku tukijadili ripoti hii ya Human Right Watch.

page 1 from 2