Synopsis
Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.
Episodes
-
Kenya : Haki ya wanahabari kuteleza majukumu yao bila vikwazo
27/07/2024 Duration: 09minJuma hili tunaangazia haki za wanahabari kupeperusha habari zao bila kuingiliwa na vyombo vya usalama katika mataifa yao. Shaba yetu bila shaka inalenga taifa la Kenya, nchi ambayo wanahabari wamejeruhiwa wakati wakitekeleza majukumu yao, ya kuangazia maandamano ya vijana wa Gen Z, ambao wamekuwa wakishinikiza mabadiliko nchini Kenya. Kwa siku sasa kilio cha wanahabari nchini Kenya kimekuwa ni kutaka serikali kuheshimu haki zao kwa kuwaruhusu kutekeleza wajibu wao bila vikwazo.Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
-
Kenya : Polisi wa Uingereza watuhumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu
16/07/2024 Duration: 09minKatika makala haya tunaangazia dhuluma zinazodaiwa kutekelezwa na wanajeshi wa Uingereza ambao wana kambi ya mazoezi nchini Kenya leo la Nanyuki. Wanajeshi hao wanadaiwa kuwabaka na kuwaua wanawake mbali na kuwacha vilipuzi katika maeneo ya mazoezi ambavyo baadaye hulipuka na kusababisha majiraha na maafa. Wanawake wambao wamekuwa na uhusiano wa kimapaenzi na wanjeshi wa uingreza eneo hilo la Nanyuki wamesumulia namna gani wamesalia na majiraha ya moyo kutokana na kuachwa na wapenzi wao wa kizungu ambao baada ya mazoezi yao, wao hurejea nchini mwao licha ya kuwazalisha.
-
Kenya : Wanaume wanapitia dhuluma za kijinsia kwenye ndoa, ila wamesalia kimya
10/07/2024 Duration: 09minVisa vya dhuluma dhidi ya wanawake vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara katika jamii mbalimbali barani Afrika na hata duniani,jambo ambalo limechangia sheria nyingi kuanzishwa kulinda wanawake,lakini hata hivyo dhuluma hizo zimeanza kuwakumba wanaume wengi kwa kunyanyaswa na kupingwa na wake wao. Katika makala haya tunaangazia dhuluma za kijinsia dhidi ya wanaume shaba yetu ikilenga taifa la Kenya, ambapo mwanahabari wetu Victor Moturi alitangamana na wanaume ambao wamehangaishwa na kudhulumiwa kwenye jamiii nchini Kenya hasa eneo la Magharibu. Kufahamu mengi skiza makala haya.
-
Sudan Kusini inakabiliwa na hali ya binadamu kutokana na wimbi kubwa la wakimbizi
06/07/2024 Duration: 09minTaifa la Sudan Kusini linashuhudia wimbi kubwa la wakimbizi wanaoendelea kukimbia vitra nchini Sudan, licha taifa hilo kuendelea kushuhudia changamoto nyingi tu ikiwemo ukosefu wa amani katika baadhi ya majimbo yake. katika makala haya tunazama kuangazia ripoti ya shirika la Care in South Sudan ambayo imechangia ripoti kuhusiana na hali ya binadamu nchini Sudan Kusini. Kufahamu mengi skiza makala haya.