Synopsis
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.
Episodes
-
Uchoraji unavyowasaidia vijana kujimudu kimaisha
16/05/2026 Duration: 20minLicha ya kuwa na Shahada ya Utafiti wa Binadamu,Sanaa ya Uchoraji imempa fursa ya kumudu Maisha, Kutana na Cletus Kenedy.
-
Sanaa ya uchoraji na Jordan Katunzi
09/05/2026 Duration: 20minMbali na kuwa na Talanta ya Uchoraji, sasa wachoraji nchini Tanzania wanasomea fani hiyo ili kufanya sanaa kwa ufanisi, Jordan Katunzi ni Mchoraji amezungumza na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.
-
John Sombi Kafula, Mwanamuziki wa muziki wa asili kutoka kabila Wasukuma
18/04/2026 Duration: 20minWasukuma ni kabila kubwa zaidi nchini Tanzania, linakadiriwa kufikia watu milioni 10, idadi inayowakilisha asilimia 16 ya wakazi wa nchi kwa ujumla, Wasukumua ni maarufu kwa Muziki wa asili.
-
Tanzania: Singeli na Mima
11/04/2026 Duration: 19minWikendi kwenye makala ya nyumba ya sanaa, Mwandishi wetu Steven Mumbi aangazia muziki wa singeli na Mima.
-
-
Uchoraji msimu wa siku kuu
28/03/2026 Duration: 19minSanaa ya uchoraji wakati wa sherehe za siku kuu katika visiwa vya Zanzibar.
-
Uigizaji Filamu na Wastara
07/03/2026 Duration: 20minUigizaji Filamu na Wastara kutoka nchini Tanzania.
-
Sanaa ya uchongaji
15/11/2025 Duration: 20minSteven Mumbi anaangazia sanaa ya uchongaji jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.
-
Real Jofu kuhusu Bongo Fleva
01/11/2025 Duration: 20minSteven Mumbi amezungumza naye msani Real Jofu kuhusu muziki wa Bongo Fleva.
-
Nyumba ya sanaa: Muziki wa densi visiwani Zanzibar
20/09/2025 Duration: 20minKatika Makala ya wiki hii tunaangazia safari ya muziki wa densi visiwani Zanzibar.
-
Vijana wa Goma wajituma kuimarisha sanaa ya muziki na utamaduni wa Afrika
17/09/2025 Duration: 20minMakala ya wiki hii imeangazia namna wasanii wanaoishi katika maeneo yenye vita mashariki mwa DRC wanavyojituma katika kuimarisha sanaa ya muziki na utamaduni wa Afrika. Mwandishi wetu Ruben Lukumbuka hivi karibuni alitembelea mji wa Goma mkowani Kivu kaskazini ambako alikutana na msanii wa muziki na mtengeneza filamu Malick Maliro ambaye anaeleza kwa urefu kuhusu mbinu zake
-
Miaka 30 ya safari ya msanii Mack el Sambo mjini Goma mashariki mwa DRC
30/08/2025 Duration: 20minHii leo ninaungana na mwenzangu Ruben Lukumbuka ambaye hivi karibuni alitembelea mji wa Goma ambako alikutana na wasanii kadhaa ambao wamo mbioni katika kuhamasisha Amani na mshikamano wa jamii kupitia Nyimbo zao, na leo kwa namna ya pekee tutaungana na msanii mkongwe wa miaka mingi katika mji huo ambaye amejiwekea sifa kubwa katika eneo la maziwa makuu MACK ELSAMBO Kataka ambaye kwa zaidi ya miaka 30 amekuwa akiimba AMANI
-
Wanamuziki mjini Goma walazimika kufanyia muziki katika nchi jirani
02/08/2025 Duration: 20minMji wa Goma mashariki ya DRC unakabiliwa na changamoto baada ya waasi wa M23 kuuchukua mji huo sasa wanamuziki wanalazimika kwenda nchi jirani kufanya Muziki. Tumezungumza naye msani Sisco laga.
-
Sanaa ya utunzi wa vitabu nchini Tanzania na Leticia Ndanzi Bubelwa
26/07/2025 Duration: 20minImezoeleka ukisikia Utunzi wa Vitabu utawazia Vitabu vya Riwaya,Tamthilia ama Hadithi ,kutana na Leticia Ndanzi Bubelwa Mtunzi wa Vitabu vya Shajara ama kwa kimombo Journals.
-
Sanaa ya Muziki na Hamis Bss
19/07/2025 Duration: 20minSanaa ya Muziki na Hamis Bss kutoka nchini Tanzania
-
Tanzania: Sanaa ya uiigizaji na Lumole Matovolwa
12/07/2025 Duration: 20minLumole Matovolwa ni Miongoni mwa waigazi wa filamu ya kwanza ya Kibiashara nchini Tanzania ya Girl Friend amezungumza na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.
-
Muziki wa Singeli nchini Tanzania
05/07/2025 Duration: 20minMuziki wa asili hubeba ujumbe unaoakisi Utamaduni wa Jamii ,kwa Tanzania Muziki wa Singeli unatajwa kuakisi Utamaduni wa Kitanzania, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Mwanamuziki wa Muziki wa Singeli Hemed Kiduku.
-
Muziki wa RNB nchini Tanzania
21/06/2025 Duration: 20minWanamuziki wachanga wajigamba kuinua muziki wa RNB kufikia malengo,Ungana na Shine 9 katika Mkala ya Nyumba ya Sanaa
-
Sanaa ya muziki wa kizazi kipya na msani Eddy Music
14/06/2025 Duration: 20minSafari ya Muziki wa kizazi kipya inaanzia mbali,sasa vijana wanalazimika kusafiri kutoka Mikoani kuja jijini Dar es salaam ili kufaulu kisanaa, Eddy Music ni msanii wa Muziki anazungumza na Steven Mumbi katika Makala haya.
-
Msanii Real Jofu asema amejifunza kuwa mvumilivu baada ya kuondoka jela
07/06/2025 Duration: 20minMara baada ya kutoka Jela Msanii Real Jofu anasema amejifunza kuwa mvumilivu ili kufikia malengo,Ungana na Steven Mumbi kaktika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Msanii huyo.