Synopsis
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.
Episodes
-
Muziki wa dansi na ule wa kizazi kipya nchini Tanzania
24/05/2025 Duration: 20minMwandishi Steven Mumbi anaangazia muziki wa dansi na ule wa kizazi kipya nchini Tanzania.
-
Msanii sweet Brown wa Beni DRC na mziki wa jamii
10/05/2025 Duration: 20minSanaa ya muziki ni dawa inayofariji na kusaidia kutuma ujumbe wa amani kwa jamii amesema msanii wa miondoko mchanganyiko Gloire Tsongo almaarufu sweet Brown fresh Leader mjini Beni katika mkowa wa Kivu kaskazini mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, katika mazungumzo maalum na mwandishi wa habari wa RFI Kiswahili Ruben Lukumbuka alipotembelea eneo hilo mwezi february mwaka huu
-
Sanaa ya Ufumaji inayotumia uzi kufuma Mavazi ya aina mbalimbali
03/05/2025 Duration: 20minSanaa ya Ufumaji ni sanaa ya Mikono inayotumia uzi kufuma Mavazi ya aina mbalimbali, kutana na Farida na Esther wasanii wanaofanya saa hizo walipozungumza na Steven mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.
-
Tanzania: Tunamuangazia Samir Kassim Rashid maarufu Samir Kinyulinyuli
26/04/2025 Duration: 20minSamir Kassim Rashid maarufu Samir Kinyulinyuli ni Msanii wa Sanaa ya Muziki aliyelazimika kukimbilia Dar es salaam akitokea Morogoro ili kufanikiwa kisanaa, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa ya Jumahili.