Noa Bongo - Afya Na Masuala Ya Jamii
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 1:43:48
- More information
Informações:
Synopsis
Vipindi vyetu vinajaribu kuwahamasisha wasikilizaji wetu vinazungumzia masuala ya afya katika jamii
Episodes
-
WHO yatangaza Ebola kuwa dharura ya kimataifa
18/07/2019 Duration: 02minShirika la afya duniani WHO, limetangaza homa ya Ebola kuwa dharura ya kimataifa ya afya ya umma. Tangazo hilo limetolewa baada ya taarifa ya kisa cha mgonjwa wa Ebola mjini Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
-
Unicef: Ndoa za utotoni zimepungua duniani
06/03/2018 Duration: 02minShirika la Watoto la Umoja wa Mataifa, Unicef limesema ndoa za utotoni zimepungua kwa kiwango kikubwa duniani, hususan katika nchi za Asia Kusini. Hata hivyo bado tatizo hilo ni kubwa Afrika ya Kusini mwa Sahara.
-
Haki za Wasichana
13/03/2014 Duration: 11minWanawake barani Afrika wamekuwa na nguvu nyingi katika miaka iliyopita na hata kushika nafasi za uongozi. Licha ya hilo, wasichana wengi bado wanapambana na ubaguzi. Safari ya kufikia usawa wa kijinsia bado ni ndefu.
-
Mimi Bado ni Binadamu - Hadithi ya Wagonjwa wa Akili Barani Afrika
12/08/2013 Duration: 11minUlemavu ni mwiko na laana miongoni mwa watu wengi barani Afrika. Hadithi hii inaelezea jinsi familia na marafiki wa watu wenye ulemavu wanavyojaribu kuelewa na kukabiliana na hali zao. Kwani ni binadamu tu kama wengine.
-
Mwana Mpotevu - Hadithi ya akinamama wanaolea watoto peke yao Barani Afrika
06/08/2013 Duration: 12minMara nyingi malezi ya mtoto huwa kazi ngumu, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha afya nzuri na elimu bora ya mtoto. Hali hii huwa ngumu zaidi hasa kwa mzazi mmoja wa kike ambaye mzigo wa kifedha na malezi umo mikononi mwake.
-
Watu wenye ulemavu – Kipindi 10 – Hadithi ya Oluanda
21/03/2011 Duration: 12minMsisimko ni mkubwa na nderemo zinasikika Maganye. Kabla kuungana na umati wa watu, tujifunze kilichomsibu Chitoto na kilichoandikwa kwenye barua ambayo wazazi wa Kangwa wanaipata.
-
Watu wenye ulemavu – Kipindi 09 – Kufanya Historia
21/03/2011 Duration: 12minKatika kipindi hiki, mengi yanaonekana yakijitokeza. Chitoto anakanyagwa na gari na bwana na Bi Mali! Na Oluanda na Kangwa wana habari mpya motomoto kwa wazazi wao. Tamthiliya yaendelea.
-
Watu wenye ulemavu – Kipindi 08 – Sio rahisi hivyo
21/03/2011 Duration: 12minBabake Kangwa, Bwana Mali anajitolea kusaidia. Mabango yamebandikwa na watu wako tayari kwa maandamano ya amani. Lakini subiri, jambo moja muhimu linakosekana. Bonyeza hapa upate kujua!
-
Watu wenye ulemavu – Kipindi 07 – Kupigania usawa
21/03/2011 Duration: 12minOluanda huenda akalazimika kukabiliana na changamoto za kutembea lakini amedhamiria kuwahimiza watu wenye ulemavu Maganye kudai haki sawa. Tuchunguze atafika umbali gani anapoendelea na mipango yake.
-
Watu wenye ulemavu – Kipindi 06 – Kufanya mabadiliko
21/03/2011 Duration: 12minMshonaji viatu mwenye mguu mmoja ambaye sasa ni maarufu, ana rafiki mpya wa karibu. Mrembo Kangwa amechochea kitu katika maisha ya Oluanda na mabadiliko yanatokea.