Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Informações:

Synopsis

Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.

Episodes

  • Mikoko: Wanawake Lamu mbioni kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

    27/11/2023 Duration: 10min

    Athari za mabadiliko ya hali ya hewa hazichagui mtoto au mtu mzima, akina mama wamelichukua kuwa jukumu lao kuhakikisha mikakati imefanikishwa katika harakati za kupunguza athari hizi haswa kupitia upanzi na uhifadhi wa mikoko Katika kijiji cha Mtangawanda, jimboni Lamu pwani ya Kenya, tunakutana na kundi la akina mama ambao kupitia mafunzo, sasa ni wakereketwa wa mazingira.Licha ya changamoto mbalimbali kukiwemo dini na hata ukataji haramu wa mikoko kutokana na umuhimu wake, kinachowatia moyo ni hatua walizopiga katika kipindi cha miaka 5 iliyopita, na hata cha ziada ni kufanikiwa kuchakata tena taka za plastiki ambazo ni hatari kwa ukuaji wa mikoko.

  • Maendeleo kidogo katika mazungumzo ya mkataba wa kukomesha uchafuzi wa plastiki

    21/11/2023 Duration: 10min

    Msikilizaji kwa juma moja, wajumbe kutoka mataifa takriban 175, walikusanyika jijini Nairobi kwa majadiliano ya awamu ya tatu kuelekea kuundwa kwa mkataba wa kisheria wa kimataifa kupambana na uchafuzi utokanao na taka za plasitki ikiwa ni pamoja na mazingira ya baharini.Katika kipindi hiki, wajumbe wa serikali na wadau wengine kutoka mashirika yasio ya kiserikali walikuwa wakijadili mapendekeo ya maudhui yanayofaa kujumuishwa kwenye mkataba huo wa kisheria.  Baadhi ya nchi zimependekeza mkataba huo kuangazia matumizi endelevu ya bidhaa za plastiki kuanzia kwenye uzalishaji hadi matumizi yake, huku zingine zikipendelea mkataba huo kuangazia suala la uchakataji na matumizi ya tena ya plastiki.Kwa kuanza makala yetu hivi leo, tunaye Henry Msuya, mjumbe wa Tanzania kwenye majadiliano ya mktababa wa kudhibiti taka za plastiki. Hapa anaanza kwa kueleza namna majadiliano yalivyokuwa wiki nzima.

page 2 from 2