Changu Chako, Chako Changu

Informações:

Synopsis

Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.

Episodes

  • Utamaduni wa kabila la Wataita na mwanamuziki Hiro le Coq katika Makala haya ya leo.

    13/11/2023 Duration: 19min

    Karibu mpenzi msikilizaji katika Makala ya leo Changu Chako Chako Changu, ambapo nakukumbusha historia na tamaduni ya watu wa kabila la wataita, na kwenye le parler francophone tutaangazia ratiba ya shughuli za kitamaduni Alliance France Francaise ya Nairobi, Dar es salaam, Arusha, na Institut francais ya Lubumbashi. Na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Hiro Le Coq rapa wa Ufaransa mwenye asili ya DRC. Mimi naitwa Ali Bilali bienvenue.

  • Mwanahabari kutoka DRC ashinda Toleo ka kumi la tuzo Ghislaine Dupont na Claude Verlon

    09/11/2023 Duration: 19min

    Makala haya yanazungumzia kuhusu tolea la 10 la tuzo ya Ghislaine Dupont na Claude Verlon ambalo hutolewa kila Novemba 02 ya kila mwaka na RFI ili kuwaenzi waandishi wa habari hao wawili waliofariki miaka 10 iliopita huko Kidal kaskazini mwa Mali baada ya kutekwa na wanajihadi, ambapo Joseph Kahongo wa (RDC) na Ange J. Agbla (Bénin) ndie washindi wa toleo hili la kumi. ambatana naye Ali Bilali kudahamu mengi zaidi.

  • Historia ya siku ya kupinga dhulma dhidi ya wanahabari na utoaji wa tuzo ya Ghislaine Dupont

    31/10/2023 Duration: 19min

    Leo Octoba 29 kwenye Makala Changu chako Chako Changu tunazungumzia kuhusu historia ya Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Kutokujali kwa Uhalifu Uliotendwa dhidi ya Wanahabari ambayo huadhimishwa kila Novemba 2. Na kwenye le parler francophone kama kawaida nitakujuza nini kinachojiri kwenye vituo vya Alliance francaise ya Nairobi, Dar es Salaam na Arusha, na kwenye Muziki ninakuletea mwanamuziki Jay Melody kutoka nchini Tanzania. Bienvenue et Bon Dimanche, yaani Karibu na Jumapili njema.

  • Siku ya kimataifa ya utamaduni nchini Kenya Octoba 10

    16/10/2023 Duration: 19min

    Karibu msikilizaji katika makala haya changu chako chako changu Jumapili ya leo ambapo Jumapili ya leo tunazungumzia kuhusu siku ya kitaifa ya utamaduni nchini Kenya ambayo huadhimishwa kila Octoba 10. Na kwenye le parler francophone tutaangazia namna shughuli za kitamaduni zinavyo pamba moto kuelekea mwisho wa mwaka Alliance Francaise ya Arusha, Nairobi na Dar es salaam na kwenye Muziki nitaungana na mwenzangu Benson Waokoli kuzungumzia kumbukumbu ya kifo cha francois Lwambo Lwanzo Maki

page 2 from 2