Wimbi La Siasa

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 4:03:44
  • More information

Informações:

Synopsis

Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa

Episodes

  • Nini hatima ya maandamano yanayoendelea nchini Kenya ?

    26/06/2024 Duration: 11min

    Siku ya Jumanne, Kenya ilishuhudia maandamano makubwa kupinga mswada tata wa sheria uliopitishwa na wabunge, kuongzeza kodi.Waandamanaji wenye hasira, walivamia majengo ya Bunge jijini Nairobi na kusababisha uharibifu, huku polisi wakiwapiga risasi na kuwauwa waandamanaji.Nini itakuwa suluhu ya mzozo huu ?Tunachambua suala hili na Majeed Ali, mmoja wa vijana wanaounga mkono waandamanaji na Oponyo Akolo Eugene, kutoka Shirika la Wazalendo Movement Afrika, anayepinga maandamano.

  • Kuapishwa kwa Cyril Ramaphona na mstakabali wa serikali mpya ya Afrika kusini

    21/06/2024 Duration: 10min

    Makala hii inaangazia mchakato wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa huko Afrika kusini, baada ya kuapishwa kwa rais Ramaphosa huku chama tawala ANC kikitangaza kufikia makubaliano na vyama vingine, kama DA. Kudadavua hili mwandishi wetu Ruben Lukumbuka anazungumza na Lugete Musa Lugete ni mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Jijini Daresalaam nchini Tanzania, pia Félix Nabel Arego, mtaalamu wa siasa wa siasa za Afrika kusini akiwa Nairobi Kenya

  • Rwanda yaanza maandalizi ya Uchaguzi Mkuu Julai 15 kumchagua rais na wabunge

    12/06/2024 Duration: 10min

    Wananchi wa Rwanda wanajiandaa kupiga kura tarehe 15 mwezi Julai kumchagua rais na wabunge.Wiki iiyopita, Tume ya Uchaguzi ilitangaza orodha ya awali ya wagombea urais ambao ni rais Paul Kagame ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1994, Frank Habineza kutoka chama cha Democratic Green na Philippe Mpayimana mgombea binafsi.Mwanasiasa na mpinzani wa Kagame, Diane Rwigara, kutoka chama cha People Salvation Movement, ombi lake lilikataliwa. Tunachambua maandalizi ya uchaguzi nchini Rwanda. Wachambuzi wetu ni Edwin Kegoli akiwa Nairobi na Mali Ali akiwa jijini Paris

  • Chama tawala nchini Kenya, kwenye njia panda migawanyiko ikishuhudiwa

    31/05/2024 Duration: 09min

    Nchini Kenya, malumbano ya kisiasa yameanza kushuhudiwa kati ya rais William Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua, malumbano hayo yametokana na tofauti za kisiasa kuelekea uchaguzi wa mwaka 2027. Kuna hofu kwamba wandani wa rais William Ruto wanawatumia wabunge vijana kutoka ngome ya naibu rais kumtatiza kisiasa hili likiibua malumbano makli ya kisiasa nchini Kenya.Benson Wakoli hapa anachambua swala hili na mchambuzi wa siasa Felix Arego.

page 2 from 2