Synopsis
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.
Episodes
-
Michezo ya olimpiki yaanza Paris Ufaransa, Siasa za Kenya, DRC na kwengineko
27/07/2024 Duration: 20minMakala imeangazia hafla ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya Paris siku ya Ijumaa ya wiki hii, huku miundombinu ya treni za umeme ikishambuliwa, rais William Ruto atangaza baraza la mawaziri akiwajumuisha wanasiasa wanne wa upinzani, kesi dhidi ya kiongozi wa muungano wa waasi Corneille Nangaa jijini Kinshasa nchini DRC, Maandamano na kukamatwa kwa vijana kule Uganda, siasa za Afrika Magharibi, na Kaskazini,Joe Biden ajijiondoa katika ki nyang’anyiro cha uchauguzi huku Kamala Harris akiteuliwa kuwa mgombea wa chama cha Demokratic nchini Marekani.
-
Ruto ateua mawaziri wapya, Paul Kagame ashinda uchaguzi, usalama bado mashariki DRC
20/07/2024 Duration: 20minMakala hii imeangazia hatua ya rais wa Kenya William Ruto ya kuwateua mawaziri wapya baada ya mashinikizo, nchi yake ikishuhudia maandamano ya vijana, Kukamatwa kwa mshukiwa wa mauaji ya watu ambao miili yao ilikutwa jalalani Kware jijini Nairobi akiri kuwaua wanawake 42, rais wa Rwanda Paul Kagame ashinda uchaguzi kwa kishindo, Waasi wa M23 na jeshi la congo FARDC wakubali kusimamisha vita baada ya Marekani kutangaza kuongeza muda wa siku 15 kuruhusu misaada ya kibinadamu...na mengineyo..kwengineko duniani ambako watu wamestushwa ulimwenguni kuhusu hitilafu iliyojitokeza kiteknolojia..-
-
Rais Ruto avunja baraza la mawaziri, uchaguzi huko Rwanda, usalama wazorota DRC
13/07/2024 Duration: 20minMakala ya yaliyojiri wiki hii imeangazia hatua ya rais wa Kenya William Ruto kulivunja baraza lake la mawaziri, huku inspekta mkuu wa polisi Japhet Koome akubali kujiuzulu, raia nchini Rwanda wajiandaa kushiriki uchaguzi mkuu wa rais na wabunge nchini Rwanda jumatatu ya julai 15, pia hali ya mapigan yashuhudiwa nchini DRC licha ya wito wa Marekani wa kusitishwa mapigano kwa sababu za kibinadamu.Hali iliyojiri kwenye nchi za Afrika magharibi na kaskazini, Ufaransa, na Marekani.
-
DRC: Wanajeshi wanaodaiwa kutoroka adui kwenye mapambano wahukumiwa
06/07/2024 Duration: 20minMiongoni mwa yale utakayosikia katika makala ya wiki hii ni pamoja na hatua ya Rais wa Kenya William Ruto kuzungumza na wapiga kura kwa njia ya mtandao wa X, wanajeshi waliotoroka adui DRC kuhukumiwa na vilevile mkutano wa nchi za Sahel zinazoongozwa na wanajeshi.