Habari Za Un

Mbinu za medani tulizopatiwa ni za kimataifa- Afisa FARDC

Informações:

Synopsis

Siku zikizidi kuhesabiwa kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, kuondoka nchini humo, ujumbe huo unaendelea kutekeleza wajibu wake wa kujengea uwezo jeshi la serikali, FARDC kuweza kukabili vikundi vilivyojihami ambavyo vinatajwa kuhusika na asilimia 65 ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo mwezi Februari mwaka huu, kwa mujibu wa ripoti ya pamoja ya Umoja wa Mataifa na serikali. Je, FARDC linajengewa uwezo gani? Assumpta Massoi anafafanua zaidi.Hapa si uwanja wa vita bali ni uwanja wa mazoezi! Wanajeshi 30 wa FARDC au jeshi la serikali nchini DRC wakiwa kwenye mafunzo  ya  kulenga shabaha. Mbele kuna karatasi lililochorwa binadamu na sasa wanatakiwa kulenga maeneo mbali mbali ya mwili yaliyowekwa alama.Ni mbinu wanazopatiwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Brazil, hapa Beni jimboni Kivu Kaskazini ili waweze kukabiliana na waasi kwenye maeneo misituni. Kapteni Rombaut Mukoka ni Afisa wa jeshi la FARDC na anasema, “Mafu