Habari Za Un

Informações:

Synopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodes

  • 11 APRILI 2024

    11/04/2024 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Alice Nderitu, Mshauri Maalum wa Umoja wa Mataifa katika kuzuia mauaji ya kimbari akiwa Kigali hivi majuzi kwenye kumbukizi anamulika nini kifanyike kuhakikisha kitendo kama hicho kinasalia historia. Pia tunakuletea muhtasari wa habari za Gaza, Sudan, Uganda na uchambuzi wa neno “PAMBAJIO”.Wakati mgogoro nchini Sudan ukiingia katika mwaka wake wa pili, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kutafuta Ukweli nchini Sudan umezitaka pande zinazokinzana zisitishe mapigano, zilinde raia na kuruhusu mtiririko wa misaada. Taarifa iliyochapishwa leo na OHCHR imemnukuu Mwenyekiti wa ujumbe huo, Mohamed Chande Othman akisema, "Pande zinazopigana Sudan zina wajibu wa kisheria kuwalinda raia, lakini zimeonesha kutojali kufanya hivyo.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limetangaza kwamba moja ya magari yake jana yakisubiri kuingia kaskazini mwa Gaza lilishambuliwa kwa risasi za moto. Pia UNICEF imechapisha katika ukurasa wake wa mtandao wa X video ya Msemaji wa

  • Jifunze Kiswahili: Pata uchambuzi wa neno “PAMBAJIO”

    11/04/2024 Duration: 01min

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili  leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania , BAKITA anafafanua maana ya neno “PAMBAJIO”.

  • Alice Nderitu: Dunia bado haijajifunza lolote kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda dhidi ya Watutsi

    09/04/2024 Duration: 06min

    Miaka 30 iliyopita mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda yaliyoishangaza, dunia yalitokea kuanzia Aprili 7 mwaka 1994 na kudumu kwa siku 100 zilioghubikwa na ukatili wa hali ya juu na mamilioni ya watu kufurushwa makwao. Tangu wakati huo Umoja wa Mataifa umekuwa mstari wa mbele kuchukua hatua kuhakikisha asilani jinamizi hilo halitokei tena popote pale duniani. Manusura wa mauaji hayo wanasemaje kuhusu kumbukumbu hii? Na je dunia imejifunza nini kutokana na mauaji hayo ya Rwanda taifa ambalo limeshafungua ukurasa mpya na kuyapa kisogo? Twende mjini Kigali ambako kumbukumbu kubwa imefanyika mwishoni mwa wiki na itaendelea kwa siku 100, shuhuda wetu ni Eugene Uwimana afisa mawasiliano wa ofisi ya mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Rwanda.

  • 09 APRILI 2024

    09/04/2024 Duration: 10min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka mjini Kigali ambako kumbukumbu ya mauaji ya kimbari imefanyika mwishoni mwa wiki na itaendelea kwa siku 100. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani tunakupeleka nchini Sudan Kusini.Baada ya huduma ya ulinzi wa amani kwa zaidi ya miaka 20 huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, walinda amani kutoka China, hii leo wameondoka kutoka kambi yao iliyoko nje kidogo ya mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini, Bukavu ambako walishiriki kwa kiasi kikubwa katika ujenzi wa miundombinu.Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Olga Sarrado Mur katika mkutano na waandishi wa habari leo mjini Geneva, Uswisi ameeleza kwamba vita nchini Sudan ikikaribia kutimiza mwaka mmoja kamili na ikiendelea kupamba moto, idadi ya Wasudan waliolazimika kukimbia sasa imepita watu milioni 8.5, huku milioni 1.8 kati yao wakiwa wamevuka mipaka ya nchi. Na kwa mujibu wa Ripo

  • Mariam Suleiman: Wanawake tuna ujuzi, tuna uweo na tunaweza

    08/04/2024 Duration: 02min

    Mwanamke akiwezeshwa anaweza, huo ndio umekuwa usemi wa Umoja wa Mataifa ukipigia chepuo wanawake kujumishwa katika kila Nyanja ya Maisha ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuchangia katika maendeleo ya jamii. Usemi huo unaungwa mkono na mwanamke mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambaye sasa anaishi Kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Kutana na Mariam Suleiman ambaye kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR anasema vita ilimfungisha virago Congo DRC hadi hapa kambini Kakuma, ingawa ilimvurugia amani yake haikumkatishia ndoto zake za kuendelea na ufundi wa kuchomelea vyuma na pia kuwa mkufunzi wa kazi hiyo.“Katika kuchomelea vyuma ninafurahia sana kufanyakazi kazi hiyo ninapokwenda kazini na kujikuta ni mwanamke peke yangu uwanjani na hivyo ninajivunia sana kwa sababu sio kazi rahisi kwenda hapo ukiwa mwanamke peke yako katikati ya wanaume 15. Hivyo ninajivunia sana kuwa mchomelea vyuma na mkufunzi wa kuchomelea na kutengeneza vyuma”Kwa Mariam ma

  • Raia nchini DRC wasimulia jinsi wanavyonufaika na miradi iliyofanikishwa na MONUSCO

    08/04/2024 Duration: 03min

    Kadri siku za MONUSCO kuondoka nchini DRC zinavyokaribia, vivyo hivyo wananchi wanufaika wa miradi iliyofanikishwa na ujumbe huo wanazidi kujitokeza kuelezea hisia zao, kwani ujumbe huo unatakiwa uwe umeondoka nchini humo mwishoni mwa mwaka huu wa 2024.Miongoni mwa wanufaika ni shule ya msingi Lubumba hapa Kamanyola na Mwalimu Mkuu Texas Chekabiri anaelezea hali ilivyokuwa. Assumpta Massoi amefuatilia na kutuelezea zaidi katika makala hii.

  • 08 APRILI 2024

    08/04/2024 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia ombi la Palestina kujiunga rasmi kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa, na uwezeshaji wa wanake ambapo tunatembelea mkimbizi katika kambi ya Kakuma nchini Kenya. Makalatunakupeleka nchini DRC na mashinani nchini Tanzania.Huko Gaza, watoa misaada ya kibinadamu wakiwa na wasiwasi mkubwa juu ya mipango ya Israel kuvamia eneo la Rafah hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa Palestina imeanza mchakato wa kuwa mwanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa kwani hivi sasa ujumbe wake ni uangalizi usioipatia hadhi ya kupiga kura. Mchakato huo unaanzia ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Mwanamke akiwezeshwa anaweza, huo ndio umekuwa usemi wa Umoja wa Mataifa ukipigia chepuo wanawake kujumishwa katika kila Nyanja ya Maisha ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuchangia katika maendeleo ya jamii. Usemi huo unaungwa mkono na mwanamke mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambaye sasa anaishi Kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Katika makala makala ambapo Assumpta Massoi

  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili ombi la Palestina kuwa mwanachama

    08/04/2024 Duration: 02min

    Huko Gaza, watoa misaada ya kibinadamu wakiwa na wasiwasi mkubwa juu ya mipango ya Israel kuvamia eneo la Rafah hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa Palestina imeanza mchakato wa kuwa mwanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa kwani hivi sasa ujumbe wake ni uangalizi usioipatia hadhi ya kupiga kura. Mchakato huo unaanzia ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Ratiba ya mikutano hii leo hapa katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa inaonesha kuwa Baraza la Usalama lenye wajumbe 15 kuanzia saa nne kamili asubuhi mpaka saa sita kamili mchana kwa saa za New York Marekani, litakutana kwanza katika kikao cha faragha na kisha kikao kitafunguliwa kwa umma kusikiliza wanapojadili ombi la Palestina kuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa.Palestina imekuwa ikishiriki katika masuala mbalimbali ndani ya Umoja wa Mataifa lakini kwa ngazi ya muangalizi na sasa uongozi wa Palestina inataka hadhi hiyo kubadilishwa na kuwa mwanachama kama wanachama wengine 193 wa Umoja wa Mataifa.Wajumbe katika baraza hilo la UN katika mazungumzo

  • UNICEF na jitihada za kuimarisha huduma za Afya ya Akili kwa vijana nchini Rwanda

    05/04/2024 Duration: 02min

    Makala hii inaeleza safari ya matumaini na uthabiti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNICEF Rwanda linaposhirikiana na Rwanda Biomedical Center (shirika kuu la kitaifa la utekelezaji wa afya lenye jukumu la kufanya utafiti wa kisayansi, kutoa huduma za uchunguzi, na kutekeleza afua za kiafya ili kulinda taifa la Rwanda dhidi ya magonjwa na matishio mengine ya kiafya) kuleta mapinduzi katika huduma za afya ya akili kwa vijana. Katika mpango huu wa kutia moyo, UNICEF inavunja vizuizi na kukuza ujasiri kwa kutoa usaidizi muhimu kama vile nasaha shuleni

  • Mlo shuleni wawawezesha wasichana kuepuka ndoa za utotoni Sudan Kusini

    05/04/2024 Duration: 03min

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP nchini Sudan Kusini kupitia programu yake ya chakula shuleni imefanikiwa kuwasaidi wasichana wengi kuepukana na ndoa za utotoni. Sudan Kusini ni moja kati ya mataifa yenye viwango vya chini vya watu wanaojua kusoma na kuandika hususani kwa wasichana. Jamii katika taifa hilo la afrika ya mashariki huwaoza mabinti ikiwa ni njia moja wapo ya familia kujipatia mali na hivyo mtoto wa kike hujikuta akikosa haki yake ya msingi ya kupata elimu.Huko Kapoeta Mashariki katika jimbo la Equatoria mashariki, shule moja ya msingi ambayo hatutaitaja jina imekuwa kimbilio la wasichana walio katka hatari ya kuolewa katika umri mdogo, mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo ni Grace mwenye umri wa miaka 16 anasema shule hiyo imekuwa nikama peponi.“Nilipokuwa kijijini, wakati baba yangu alikuwa hai, maisha yalikuwa sawa na nilifurahia kila kitu maishani. Lakini mara baada ya baba yangu kufariki, hapo ndipo maisha yangu yakawa magumu, kaka yangu alitaka niolewe katika umri mdo

  • 05 APRILI 2024

    05/04/2024 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia vita katika Ukanda wa Gaza ukielekea miezi siti hapo kesho, na programu ya mlo shuleni nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Rwanda na mashinani nchini DRC, kulikoni?”.Kesho kutwa jumapili ikiwa ndio itatimu miezi sita ya mzozo wa Gaza, huko Mashariki ya Kati, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo amezungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani akirejelea wito wake wa sitisho la mapigano kwa misinigi ya kiutu, kuachiliwa kwa mateka wote bila masharti, ulinzi wa raia na misaada ya kiutu ifikie walengwa bila vikwazo vyovyote huku akikgusia pia Israeli kutumia akili mnemba kwenye operesheni zake.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP nchini Sudan Kusini kupitia programu yake ya chakula shuleni imefanikiwa kuwasaidi wasichana wengi kuepukana na ndoa za utotoni. Katika makala Anold Kayanda anatupeleka nchini Rwanda kusikia programu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF Rwanda kudhibiti tatizo la changa

  • Kuelekea miezi 6 ya mzozo wa Gaza, Guterres apinga matumizi ya akili mnemba kusaka wahalifu

    05/04/2024 Duration: 02min

    Kesho kutwa jumapili ikiwa ndio itatimu miezi sita ya mzozo wa Gaza, huko Mashariki ya Kati, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo amezungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani akirejelea wito wake wa sitisho la mapigano kwa misinigi ya kiutu, kuachiliwa kwa mateka wote bila masharti, ulinzi wa raia na misaada ya kiutu ifikie walengwa bila vikwazo vyovyote huku akikgusia pia Israeli kutumia akili mnemba kwenye operesheni zake. Guterres akianza hotuba yake kwa kuelezea kuwa Jumapili hii inatimu miezi sita tangu mashambulizi hayo na kuelezea kuwa tarehe 7 Oktoba ni siku ya machungu kwa Israel na dunia, kwani Umoja wa Mataifa na yeye binafsi wanaomboleza vifo vya waisrael 1,200 waliouawa hadi sasa. Hakuna kinachohalalisha mashambulizi yale ya Hamas, amesema Guterres akisema pia katika kipindi cha miezi sita pia wapalestina zaidi ya 32,000 wameuawa na wengine zaid iya 75,000 wamejeruhiwa. Maisha ya watu yametwamishwa na heshima ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu imesambaratishw

  • Ujumuishwaji wa wanawake katika huduma za kifedha ni muhimu - Nangi Massawe, Benki Kuu Tanzania

    04/04/2024 Duration: 10min

    Lengo namba 5 la maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa au SDG5 linahimiza kila nchi kuhakikisha wanawake wanawezeshwa na kujumuishwa katika kila nyanja ya Maisha ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 hawasalii nyuma katika maendeleo.Moja ya masuala yanayotiliwa msukumo zaidi hivi sasa ni ujumuishwaji wa wanwake katika masuala ya huduma za kifedha n anchi nyingi zimeanza kuchukua hatua ikiwemo Tanzania. Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili amezungumza na Nangi Moses Massawe kutoka Benki Kuu ya Tanzania ambaye ni meneja wa kitengo cha huduma jumuishi za kifedha. 

  • Jifunze Kiswahili: Tofauti ya maneno “Adhuhuri na Alasiri.”

    04/04/2024 Duration: 01min

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adhuhuri na Alasiri.”

  • 04 APRILI 2024

    04/04/2024 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia ujumuishwaji wa wanawake katika masuala ya kifedha kwa lengo la kutimiza lengo la Umoja wa Mataifa la usawa wa kijinsia katika Nyanja zote. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na katika kujifunza kiswahili tunakuletea ufafanuzi na tofauti ya maneno “Adhuhuri na Alasiri”.Leo ni siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na msaada wa kuchukua hatua dhidi ya mabomu hayo. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mabomu, vilipuzi na vifaa vingine vya mlipuko vinaendelea kuua na kujeruhi watu katika maeneo mengi yenye changamoto kubwa za migogoro duniani na matokeo yake vifaa hivyo vya mlipuko, kwa wastani hukatili maisha ya mtu mmoja kila saa, na waathirika wakubwa wakiwa ni watoto.Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, Jamie McGoldrick anaelekea Gaza leo. Umoja wa Mataifa unaeleza  kuwa mapigano makali kati ya wanajeshi wa Israel na makundi yenye silaha ya Palestina yanaendelea kur

  • UNCTAD, UNECA, Kenya kuunda viashirio vipya vya kupima usawa wa kijinsia katika sekta ya biashara.

    03/04/2024 Duration: 03min

    Umoja wa Mataifa umekuwa ukipigia upatu lengo namba tano la Malengo Endelevu ya Umoja huo linalohimiza usawa kwa wote katika nyanja zote ifikapo mwaka 2030. Hata hivyo ili kuelewa jinsi biashara inavyoathiri wanaume na wanawake ni muhimu kuunda sera za biashara zinazojumuisha zaidi na zenye usawa ambazo zinakuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa kiuchumi kwa wote,hii inahitaji takwimu nzuri za kitaifa kuhusu jinsia katika biashara.Kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD na Tume ya Umoja wa Mataifa ya Kiuchumi ya Afrika UNECA, Kenya inaunda viashirio vipya vya kupima usawa wa kijinsia katika sekta ya biashara. Evarist Mapesa amefuatilia taarifa hiyo kwa kina na kutuandalia makala hii. 

  • Mbinu za medani tulizopatiwa ni za kimataifa- Afisa FARDC

    03/04/2024 Duration: 02min

    Siku zikizidi kuhesabiwa kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, kuondoka nchini humo, ujumbe huo unaendelea kutekeleza wajibu wake wa kujengea uwezo jeshi la serikali, FARDC kuweza kukabili vikundi vilivyojihami ambavyo vinatajwa kuhusika na asilimia 65 ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo mwezi Februari mwaka huu, kwa mujibu wa ripoti ya pamoja ya Umoja wa Mataifa na serikali. Je, FARDC linajengewa uwezo gani? Assumpta Massoi anafafanua zaidi.Hapa si uwanja wa vita bali ni uwanja wa mazoezi! Wanajeshi 30 wa FARDC au jeshi la serikali nchini DRC wakiwa kwenye mafunzo  ya  kulenga shabaha. Mbele kuna karatasi lililochorwa binadamu na sasa wanatakiwa kulenga maeneo mbali mbali ya mwili yaliyowekwa alama.Ni mbinu wanazopatiwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Brazil, hapa Beni jimboni Kivu Kaskazini ili waweze kukabiliana na waasi kwenye maeneo misituni. Kapteni Rombaut Mukoka ni Afisa wa jeshi la FARDC na anasema, “Mafu

  • 03 APRILI 2024

    03/04/2024 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala inatupeleka nchini kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo kwa mara nyingine yameonya kwamba bila dalili zozote za usitishaji mapigano Gaza hali ya kibinadamu inaendelea kuwa janga huku mashambulizi ya Israel yakiendelea kukatili maisha, kufurusha watu na kusababisha uharibifu usioelezeka na njaa nayo ikiongeza hofu ya hatma ya watu wa eneo hilo.Siku zikizidi kuhesabiwa kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, kuondoka nchini humo, ujumbe huo unaendelea kutekeleza wajibu wake wa kujengea uwezo jeshi la serikali, FARDC kuweza kukabili vikundi vilivyojihami ambavyo vinatajwa kuhusika na asilimia 65 ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo mwezi Februari mwaka huu, kwa mujibu wa ripoti ya pamoja ya Umoja wa Mataifa na serikali. Makala inatupeleka nch

  • UN - Bila usitishaji mapigano hali ya kibinadamu inaendelea kuwa tete Gaza

    03/04/2024 Duration: 02min

    Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo kwa mara nyingine yameonya kwamba bila dalili zozote za usitishaji mapigano Gaza hali ya kibinadamu inaendelea kuwa janga huku mashambulizi ya Israel yakiendelea kukatili maisha, kufurusha watu na kusababisha uharibifu usioelezeka na njaa nayo ikiongeza hofu ya hatma ya watu wa eneo hilo. Asante Anold kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA usiku wa kuamkia leo makombora ya Israel yameendelea kuvurumishwa kuelekea Gaza Kaskazini, Khan Younis na Rafah ambako takriban Wapalestina milioni 1.2 sasa wanaishi katika makazi rasmi na yasiyo rasmi na hivyo kuwaongezea hofu ya mustakbali wa maisha yao.Pia shirika hilo linasema fursa ya kufikisha misaada ya kibinadamu kwa wenye uhitaji mkubwa bado ni mtihani hasa kutokana na mamlaka ya Israel kuendelea kulinyima vibali shirika la UNRWA kufikisha msaada muhimu wa chakula na mahitaji mengine hasa Gaza Kaskazini.Hatua hiyo kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misa

  • Bado kazi ipo kupigania haki za mwanamke kote duniani - Paulina Ngurumwa

    02/04/2024 Duration: 05min

    Kinara wa elimu nchini Tanzania Paulina Ngurumwa anasema bado kazi ipo kupigania haki za mwanamke kwa hiyo harakati hizo hazitakiwi kupoa. Paulina Ngurumwa ni mwanaharakati wa haki za kijamii kupitia shirika la KINNAPA Development Programme. KINNAPA Development Programme ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa na wanajamii ya Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara, kaskazini mwa Tanzania likiwa ni chombo cha kutatua matatizo yao hasa ya ardhi. Shirika hili lilianzishwa mwaka 1992 na kwa miaka hiyo yote linajivunia kuendelea kufanikisha malengo yake na sasa hata limepanua mawanda ya huduma zake kama anavyoeleza mmoja wa viongozi Paulina Nguruma, katika mahojiano aliyoyafanya na Anold Kayanda wa Idhaa hii hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa. 

page 1 from 5