Jukwaa La Michezo

Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2027 zitafanyika Juni-Julai

Informações:

Synopsis

Leo tumeangazia CAF kudhibitisha kuwa AFCON 2027 itaandaliwa Afrika Mashariki licha ya tetesi za kuahirishwa au kuhamishwa, uchambuzi wa raundi ya mwisho ya hatua ya makundi mechi za klabu bingwa, mechi za kufuzu kombe la dunia la wasichana U20, siku ya kwanza ya michuano ya raga ya wachezaji saba kila upande divisheni ya pili ya HSBC, mfumo mpya wa mashindano ya Tour du Rwanda, kiungo wa Ghana Thomas Partey akumbwa na shtaka jipya lakini pia michezo ya Olimpiki msimu wa baridi.