Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Mwanzo mpya: vijana wa Pwani ya Kenya wajijenga upya kupitia kazi za mazingira

Informações:

Synopsis

Katika miji ya pwani ya Kenya, vita dhidi ya uraibu vimepata mwelekeo mpya wa kusisimua. Kupitia miradi ya kimazingira, vijana kutoka vituo vya kuwarekebisha tabia hawajizuia tu na mihadarati, bali wanabadili jamii zao pia kupitia miradi hiyo. Mwanahabari wetu Victor Moturi alitembelea  Mtopanga, Kaunti ya Mombasa, ambako vijana wamepata matumaini kutokana na utunzaji wa  mazingira huku wakipata riziki.