Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Mazungumzo ya amani kuhusu Sudan Kusini yamerejelewa jijini Nairobi, Kenya

Informações:

Synopsis

Katika makala ya wiki hii baadhi ya matukio ya ulimwengu tutakayoangazia ni mazungumzo ya kutafuta amani nchini Sudan Kusini ambayo yalianza Alhamisi jijini Nairobi, lakini pia madaktari nchini Kenya kusitisha mgomo wa siku 56, vilevile kule DRC, shirika la OCHA kusema kuongezeka kwa mapigano huko Kivu Kaskazini kumesababisha wimbi jipya la watu kuyahama makazi yao. Nchi ya Chad, ina rais mpya ambaye alikuwa kiongozi wa kijeshi Mahamat Idriss Deby Itno, kadhalika tutaangazia hali kule Gaza na nchini Ukraine.