Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Jamii katika Pwani ya Kenya inavyotumia mswaki "Toothbrush" kurejesha mifumoikilojia ya matumbawe

Informações:

Synopsis

Mkutano wa mazingira wa kimataifa COP28 unaendelea jijini Dubai, Saudi Arabia, lengo lake likiwa ni kuangazia namna ya dunia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Katika muktadha huo, mifumoikolojia ya bahari, ni nguzo muhimu katika kuisaidia dunia kuafikia lengo hili, kutokana na sababu kuwa bahari inasaidia kufyonza  asilimia 25 ya hewa ya kaboni.Hata hivyo, ongezeko la utoaji wa gesi hamijoto umeathiri pakubwa mifumoikolojia ya bahari zetu.Katika makala yetu hivi leo, tunatupia jicho namna jamii eneo la Pwani ya Kenya zinajihusisha na shughuli za urejesho wa mifumoikilojia ya matumbawe.