Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Hatua zitakazochukuliwa baada ya azimio la pamoja la COP28 huko Dubai

Informações:

Synopsis

Mkutano wa COP28 uliafikia mataifa mbalimbali kuanza polepole kuachana na matumizi ya mafuta ya kisukuku, mataifa ya Afrika yakitoa wito wa mataifa yenye nguvu na yanayozalisha nishati hii kwa wingi kuwa mfano katika utekelezwaji wa hilo. Mwenyekiti wa shirika la vijana la Youth Survival Organization, YSO, linalojihusisha pia na mzingira, Humphrey Mrema kutoka nchini Tanzania, anaangazia jinsi mkutano wa COP28 ulivyokuwa na mambo yanayoweza kutekelezwa na nchi kufikia mwaka 2030 lakini pia mwaka 2050.