Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Mbinu za kiasili ili kukabiliana na changamoto za kijamii na hali ya hewa

Informações:

Synopsis

Suluhu za kiasili zinashirikisha hatua mbalimbali za kulinda na kurejesha mandhari ya bahari, maeneo ya maji na maeneo ya mijini ili viumbe hai waweze kukabiliana na changamoto kama vile usalama wa chakula na maji, mabadiliko ya hali ya hewa, hatari za maafa na afya ya binadamu. Suluhu hizi zinasaidia urejesho wa misitu, ardhioevu na pia kuabdili mbinu za kilimo zinazosaidia udongo wenye afya.Kuangazia suluhu hizi za kiasili katika mabadiliko ya hali ya hewa, tunaungana naye Fredrick Kihara, Mkurugenzi wa hazina ya maji Afrika katika shirika la The Nature Conservancy, TNC, nchini Kenya.